Wafanyakazi wa misaada watekwa, dereva auliwa huko Dadaab

Juni 29, 2012

  • 1 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Watu wenye silaha waliua si chini ya mtu mmoja na kuteka nyara wafanyakazi wanne wa misaada katika makambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya karibu na mpaka wa Somalia siku ya Ijumaa (tarehe 29 Juni), AFP iliripoti.

“Wafanyakazi wane wa misaada walitekwa nyara wakiwa na dereva wao, ambaye inawezekana alikuwa Mkenya,” Naibu Afisa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini mashariki ya Kenya Philip Ndolo aliiambia AFP.

Mateka hao wanatoka Canada, Norway, Pakistani na Ufilipino, alisema.

Polisi wanawatafuta wenye silaha hao. Ambao waliondoka na mateka katika gari yao.

Maafisa wa afya wa shirika la misaada la Ujerumani GIZ alisema dereva wa Baraza la Wakimbizi la Norway (NRC) aliuwawa na askari wawili walijeruhiwa katika shambulio hilo, lililotokea katika kambi kubwa ya Ifo 2 mnamo saa za mchana.

“Mmoja wa wafanyakazi wa NRC aliuwawa, na wengine wawili walijeruhiwa,” alisema Faiysal Abdullahi, afisa wa afya wa GIZ.

Utekaji nyara ni la mwisho katika mfululizo wa mashambulizi katika kambi ya Dadaab, ambako watu wenye silaha mwezi wa Oktoba mwaka jana walitekwa Wahispania wawili waliokuwa wanafanyakazi na Madaktari Wasio na Mipaka. Bado wanashikiiwa mateka nchini Somalia.

Kambi kubwa ya Dadaab ni kambi kubwa zaidi uimwenguni, yenye wakazi zaidi ya 465,000 mpaka mwisho wa mwezi wa Mei.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • mujaahid
    June 30, 2012 @ 03:23:14AM

    Makafiri al-Shabaab wameanza kuvunjika. Mungu ni Mkubwa.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo