Kampuni ya Kijerumani kujenga kinu cha umeme nchini Kenya

Juni 25, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Kampuni ya uhandisi ya Kijerumani imetia saini mkataba wa kujenga kinu cha umeme cha megawati 95 katika mji wa Kenya wa Thika, gazeti la Business Daily la Kenya liliripoti hapo Jumapili (tarehe 24 Juni).

Kampuni ya MAN Diesel & Turbo, tawi la Volkswagen AG, litajenga kinu cha umeme cha dizeli chenye thamani ya shilingi bilioni 12 (dola za Kimarekani milioni 143). Kampuni hiyo ilitia saini mkataba pamoja na mwenye mradi huo, Kampuni ya Thika Power Limited, kitengo cha kampuni ya Matelec Group cha Lebanon.

Kinu hicho kinatarajiwa kuzalisha megawati 88 za umeme na joto linalopotea kutoka injini hizo zitatumika katika bomba ya mvuke ili kutoa megawati 6.8 zaidi za umeme. Umeme utakaozalishwa katika kinu hicho utauzwa kwa kampuni ya Kenya Power ili kuingizwa katika gridi ya taifa.

MAN Diesel & Turbo tayari imeanza kazi katika ujenzi huo, ambao unatarajiwa kuzalisha umeme mwaka ujao.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 1)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo