Juni 25, 2012
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) imeisifu Tanzania kwa kuwapatia makazi wakimbizi kutoka ukanda huo na kuimarisha amani na utulivu, gazeti la The Guardian la Tanzania liliripoti siku ya Jumatatu (tarehe 25 Juni).
Mkabala wa serikali wa kushughulikia changamoto zinazoletwa na wakimbizi zimesaidia kupunguza idadi ya wakimbizi nchini Tanzania kufikia 134,940, huku 500,000 wakiwa wamerejea makwao, kaimu mwakilishi wa UNHCR nchini Chansa Kapaya alisema katika maadhimisho ya Siku ya Wakimbizi Duniani mjini Dar es Salaam wiki iliyopita.
Kapaya aliusifu uamuzi wa serikali wa mwaka 2010 wa kuwapa uraia wakimbizi 162,000 wa Burundi waliokuwa wameishi Tanzania kwa zaidi ya miaka 40.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alisisitiza umuhimu wa nchi kuwapatia hifadhi wasiokuwa na makazi.
"Ni lazima tufanye kazi kwa pamoja ili kuhamasisha dhamira ya kisiasa na uongozi kuzuia na kukomesha migogoro inayoleta mtiririko wa wakimbizi," alisema. "Mahali pa kurejesha usalama, ni lazima tukabiliane na vyanzo vya msingi vya mgogoro, ili kurahisisha urejeshwaji endelevu wa wakimbizi kwa kuwapatia maisha mazuri, huduma na utawala wa sheria."
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
Mahakama moja ya Bosaso iliwatia hatiani na kuwapiga faini Wairani 78 siku ya Jumapili (tarehe 19...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata watuhumiwa 15 kuhusiana na kulichoma Kanisa la Bethania kweny...
Mkuu wa Polisi wa Kenya, David Kimaiyo, ameondoa nafasi za afisa polisi wa jimbo, afisa wa upelel...
Watu wenye silaha waliwaua watu wawili na kuwajeruhi wengine wanne katika mashambulizi tofauti kw...
Mkutano wa kuzungumzia uwezekano wa uchimbaji mafuta na gesi, uwekezaji, usalama na miundombinu n...
Wizara ya Masuala ya Wanawake na Familia ya Puntland ilianza mafunzo ya siku nane hapo Juampili (...
Zaidi ya Wasomali milioni 1 hawatakuwa na "usalama wa chakula" hadi mwezi wa Septemba, Mtandao wa...
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji