Juni 25, 2012
Bunge la Kenya litaanzisha sheria mpya ya kupinga ugaidi katika wiki zijazo ambayo itawafunga maisha gerezani watu watakaohusika katika matukio ya ugaidi, Redio Capital FM iliripoti siku ya Jumapili (tarehe 24 Juni).
Mswada wa Kuzuia Ugaidi wa mwaka 2012 ulianzishwa awali mwaka 2003 na baadaye ulifutwa baada ya fujo zilizosababishwa na baadhi ya vifungu vilivyopingwa na baadhi ya vikundi vya Kiislamu.
Lakini mwenyekiti wa Muunganiko wa Taasisi za Kiislamu Sheikh Athman Mponda alisema taasisi inaunga mkono mswada mpya na kuikana dhana kwamba ni moja ya njia ya kukandamiza Uislamu.
"Tuanaunga mkono mswada, tumeupitia na umezingatia nyanja zote. Hauna ubaguzi kwa jamii ya Kiislamu," Mponda aliwaeleza waandishi wa habari huko Nairobi.
Mponda alisisitiza kuwa dini haina maana kubwa katika vurugu inayoendelea huko Somalia.
"Tumesikia vijana wengi wa kiume wakisafiri kuelekea Somalia kupigana kile wanachokiita vita vya kidini. "Kwa nini wajihusishe katika vita na kudai kwamba wanajiunga na vita vya kidini? Hakuna mahali popote katika Qur'an palipoeleza kwamba mtu anaweza kumuua mtu mwingine au kujiua mwenyewe, kwa hivyo kwa nini watu wajihusishe na mabomu ya kujitoa muhanga?"
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
Watu watano waliuawa na wanne kujeruhiwa katika mashambulizi mawili kwenye eneo la kaskazini mash...
Sababu kuu ya vurugu ambazo ziliua zaidi ya watu 150 katika Delta ya Mto Tana mwaka jana ilitokan...
Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza mlipuko wa polio katika Pembe ya Afrika siku ya Jumatan...
Majeshi ya serikali ya Somalia yamezifungia kampuni za mawasiliano ya simu na biashara nyingine h...
Serikali ya Somalia itaanza kuunda tawala za kikanda katika maeneo yaliyokombolewa kutoka kwa al-...
Waziri wa Nishati wa Djibouti Ali Yacoub Mohamoud na Balozi wa Japani nchini Djibouti Atsushi Nis...
Ufunguzi wa Mkutano wa Wasambazaji wa mafuta na gesi Tanzania utafanyika huko Dar es Salaam tareh...
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Sijawahi kusikia kikundi hiki kinaonekana kuwa ni msemaji wa serikali ili kuhalalisha matendo yake.