Juni 25, 2012
Jeshi la Somalia litaongeza operesheni dhidi ya al-Shabaab nchini kote, Waziri wa Ulinzi Hussein Arab Isse alisema Jumatatu (tarehe 25 Juni).
Akiandamana na Kamanda wa jeshi la Somalia Abdulqadir Sheikh Ali Dini, Isse alikagua kambi za jeshi huko Mogadishu siku ya Jumapili na kupata maelezo kuhusu hali ya mafunzo, Shirika la Habari la Taifa liripoti. Waziri alisema alipata moyo kuwaona wanajeshi wa Somalia wakiwa tayari kuitetea nchi yao na kuwa tayari kufundishwa nchini.
Isse aliwapongeza wanajeshi wa Somalia na wanajeshi wa Umoja wa Afrika kwa maendeleo waliyoyafikia hadi sasa na kurudia kusema uwajibikaji wa serikali katika kuwaondoa al-Shabaab kutoka Somalia ya Kusini na ya Kati ili kurejesha amri na amani nchini, haya yalielezwa na Mtandao wa Shabelle Media Network ya Somalia.
Baadhi ya wabunge wa Somalia wameitupilia mbali hoja ya kumtaka waziri mkuu na baraza lake la maw...
Wabunge wa upinzani walidai kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikibana uhuru wa kujieleza na kud...
Sampuli ya DNA iliyochukuliwa kwenye mswaki uliokuwemo kwenye begi lililokuwa na risasi lililopat...
Wakenya kumi na wasaba wameshtakiwa kwa kuvunja amani, kufanya ghasia na ukatili dhidi ya wanyama...
Al-Shabaab imedai kuhusika na urushwaji wa makombora kwenye kasri ya rais mjini Mogadishu siku ya...
Wanajeshi wa Uganda wa Kikosi Namba 9+ wanarudi nyumbani baada ya kukamilisha miezi 13 ya ziara y...
Kikosi cha polisi cha Kenya kitaanza uhakiki wa kina wa maofisa mwezi ujao, kikianza na kusaili w...
Ujambazi ulizuiwa katika ofisi za usalama za Wells Fargo huko Mombasa ulisababisha kifo cha watu ...
Rais wa Ghana John Dramani Mahama aliahidi msaada wa nchi yake katika kipindi cha ujenzi mpya wa ...
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Al-Shabaab wako katika ukingo wa kushindwa na kuangamizwa kwao kutaleta matumaini kwa Somalia. Kwa miongo sasa nchi hii imekuwa ikipambana na umasikini na vita vya wenyewe kwa wenyewe na sasa ni wakati wa kunyanyuka kutokana na yote hayo. Sasa, ni kwa namna gani kushindwa kwa al-Shabaab kunaweza kusaidia kuijenga Somalia? Sote tunajua kuwa wawekezaji wawe au ndani au wa nje wanadhamana katika kuchangia maendeleo ya nchi. Kutokana na al-Shabaab kwisha ondoka, wawekezaji wengi watakuwa na imani ya kuwekeza pesa zao nchini. Kuangamizwa kwa al-Shabaab pia kutawawezesha wenyeji kujihusisha na shughuli za kujipatia fedha na kuimarisha uchumi wao. Wakimbizi wote hawa ambao wamekimbia kwa sababu ya vita watarejea na kujiunga na wengine katika kujenga taifa lao. Wakati tishio la al-Shabaab litapokuwa limeondolewa wafadhili watakuwa na imani na wataisaidia Somalia kukua katika masuala ya miundombinu na kuimarisha hali za maisha. Watu watakuwa na imani zaidi na kufanyakazi kuelekea lengo moja ambalo ni kuijenga Somalia.