Juni 25, 2012
Shambulio la bomu katika baa mji wa bandari wa Mombasa huko Kenya Jumapili (tarehe 24 Juni) liliua watu watatu na kujeruhi 30, kwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya na maofisa wa polisi.
Waathirika walipelekwa katika hospitali iliyo karibu wakati polisi na kitengo dhidi ya ugaidi na uchunguzi wa uhalifu kikianza ukaguzi katika eneo hilo, gazeti la Daily Nation la Kenya liliripoti.
Mlipuko ulitokea Jericho Beer Garden katika Wilaya ya Mishomoroni, ambapo mashabiki wa mpira wa miguu walikuwa wakiangalia mechi ya robo fainali ya Euro 2012 kati ya Uingereza na Italia, AFP iliripoti.
“Waathirika wawili walifariki wakiwa hospitalini. Mmoja alifariki kabla katika eneo la tukio,” alisema msemaji wa Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya Nelly Muluka.
Mkuu wa Polisi wa Jimbo Aggrey Adoli alisema mmoja wa waliojeruhiwa anashikiliwa kama mshukiwa. Mmoja kati ya watu waliojeruhiwa anatusaidia kwa sababu alitoa kauli ya kuchanganya,” alisema.
Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo.
Kenya imekuwa ikishuhudia mashambulio kadhaa ya kigaidi toka ilipozindua kampeni ya kijeshi dhidi ya al-Shabaab katika nchi jirani ya Somalia mwaka uliopita, ikiwa ni pamoja na shambulio la mgahawa wa Mombasa mwezi Mei.
Mlipuko wa Jumapili umekuja baada ya serikali ya Marekani kutoa tahadhari ya tishio la shambulio la kigaidi lililo karibu kutokea huko Mombasa.” Ubalozi wa Ufaransa huko Nairobi pia ulitahadharisha raia kuwa waangalifu sana,” huko Mombasa na maeneo yanayozunguka eneo hilo.
Tahadhari hiyo imekuja baada ya polisi wa Kenya kusema kuwa imewashikilia raia wawili wa Irani Jumatano na Alhamisi kuhusiana na kushukiwa kuwa na uhusiano na mtandao wa kigaidi unaopanga kulipua mabomu Mombasa na Nairobi, AFP iliripoti.
Mkuu wa Uchunguzi wa Uhalifu Ambrose Munyasia alisema polisi wa jimbo la Pwani walikuwa katika "tahadhari kubwa”.
“Tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha watu katika Pwani wako salama,” alisema Jumamosi. “Tumeimarisha usalama lakini tunatoa wito kwa wananchi kufanya kazi kwa karibu na sisi katika kutupa taarifa.”
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
Ukiritimba na ukosefu wa ufanisi katika bandari ya Dar es Salaam unaigharimu Tanzania na nchi jir...
Viongozi wa mkoa wa Puntland walikutana siku ya Jumanne (tarehe 21 Mei) kuwashajiisha wanawake ku...
Wanajeshi wa Somalia na wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) waliwakamata zaidi ...
Rais Ismail Omar Guelleh wa Djibouti alijadiliana ushirikiano wa kimkakati na Kanali Saleh Ben Na...
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, vikosi vya usalama na mahakama vinapaswa kuomba radhi hadharani kut...
Waziri Mkuu wa Djibouti Abdoulkader Kamil Mohamed alitoa wito wa kuongezwa kwa ushirikiano katika...
Baadhi ya wabunge wa Somalia wameitupilia mbali hoja ya kumtaka waziri mkuu na baraza lake la maw...
Wabunge wa upinzani walidai kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikibana uhuru wa kujieleza na kud...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Napenda
Oh Mwenyezi Mungu, mpaka lini wahalifu hawa watashambulia watu!!!! Mwenyezi Mungu atawasaidia watu na watawashinda magaidi kwa uhakika, hili ni suala la wakati tu.
NSIS imelala kabisa. Inakuwaje kuwa tahadhari imetolewa na watu wa nje wakati NSIS hawana habari na baadaye shambulio linatokea kama ilivyoelezwa kabla, ikiwa wao hawakuwa wamelala?