Jeshi la Kenya lajitayarisha na mashambulizi ya Kismayo

Juni 22, 2012

  • 5 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Jeshi la Kenya, linaloungwa mkono na wanamgambo wa upande wa serikali, wanajitayarisha na shambulio la kuuteka mji wa Somalia wa Kismayo, gazeti la Daily Nation la Kenya liliripoti Alhamis (tarehe 21 Juni).

"Haitakuwa vigumu kuuteka mji wa Kismayo," alisema Sheikh Ahmed Madobe, kiongozi wa Brigedia ya kijeshi ya Raslamboni ambalo linapigana pamoja na jeshi la Kenya. "[Wapiganaji wa al-Shabaab] wanakimbia, morali yao iko chini na ni suala la wakati tu kabla ya kufukuzwa kabisa kutoka kusini ya Somalia."

Wakati halisi bado haujatangazwa kwa umma lakini Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Kenya Jenerali Julius Karangi na Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga walisema mji wa bandari utaanguka mwezi Agosti.

Viongozi wakuu wa al-Shabaab, hasa wapiganaji wa kigeni ambao walikuwa wanatoa msaada wa kifedha na vifaa, wanaripotiwa kukimbia Kismayo wakielekea kaskazini kwenda Somaliland au kuvuka bahari kwenda Yemen.

Mkuu wa kikosi cha Kenya huko Afmadow Luteni Kanali Jeff Nyaga alisema hakuna kitakachofanyika kuelekea Kismayo kabla ya usalama wa Afmadow, ambayo ilitekwa mwezi uliopita wa Mei, umeimarishwa kabisa.

"Kismayo ni muhimu na tutafika hapa. Lakini operesheni itafanyika kiintelijensia," alisema. "Kwanza, lazima tuhakikishe kuwa tumeondosha vitisho vyote vya al-Shabaab katika maeneo tuliyoyagomboa."

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 40)

Dislike_icon(6)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • wycliffe onyango
    September 3, 2012 @ 10:20:15AM

    ENDELEENI NA MWELEKEO HUO WA GUNG-HO.

  • khamisi
    June 24, 2012 @ 01:02:07AM

    Ninaamini habari hii ni ya faraja sana kwa watu wa Kismayo, Somalia, Kenya na ulimwenguni kote, hasa kwa wale wanaoamini kuishi pamoja kwa amani. Wakati mipango ikiendelea, ninaomba usalama kwa watu wa Kismayo. Mwenyezi Mungu awalinde kutoka mikono ya wanaojipendelea wenyewe wanaotumia dini kwa kujitukuza wenyewe tu.

  • Omandi
    June 23, 2012 @ 08:15:07AM

    Ninafuraha kuandika hapa kuwa sisi kama Wakenya tunajivunia sana na mkabala na maendeleo yanayofanywa na vikosi vyetu nchini Somalia. Hongera kwa wasichana na wavulana wetu waliovaa sare…Tunaelewa kuwa jeshi letu limechagua mkabala wa polepole, mgumu na wa hatari katika vita vya Somalia, Tofauti na vinavyofanya vikosi vya Magharibi huko Iraki, Libya na Afghanistan…Hii ndio sababu vikosi vya Kenya viko katika darasa yao wenyewe. Msijali na maoni ya vijembe kutoka vyombo vya habari vya Magharibi na watoa maoni wao ambao daima hawawekeni katika mistari ya juu ya habari zao.., mwisho vita vitakapomaliza na historia huandikwa,tutaishi kwa amani na dada na kaka zetu wa Somalia bila ya kujiangalia mabegani kwa kujidai. Dunia itashangaa kwa nini Somalia haukugeuka kuwa kama Afghanistani au Libya. Nyinyi ni wazuri zaidi, ni hekaya inayoishi. Mngeweza kuchagua njia rahisi kama ile ya vikosi vya Ufaransa nchini Libya, kupiga mabomu kila kitu kinachoonekana na na kurejea salaam katika kambi zenu nchini Kenya. Lakini nyinyi HAPANA. Mko Somlaia sio kuua bali kuleta amani, sio kuleta vita bali kusitisha vita, sio kuigawa nchi bali kujenga ujirani wenye utulivu. IDUMU KENYA, LIDUMU JESHI LETU, IDUMU AMANI!!!

  • Ndemomandi
    June 23, 2012 @ 07:05:05AM

    Ndiyo Ndiyo! na Ndio!. Kusonga mbele bila kuhakikisha amani katika maeneo yaliyokombolewa itakuwa ni mipango ya kushindwa. Amani si rahisi na ninarejea tena, ulimwengu ujue kuwa jeshi la Kenya liko darasa la peke yao na linafanyakazi kitaaluma kwa mujibu wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Angalieni nini majeshi ya Magharibi yalivyofanya huko Libya, Iraki na Afghanistan! Daima wako katika haraka za kudondosha mabomu makubwa-wakati mwingine juu ya vijiji vya raia maskini na kurejea salama makambini mwao huku nyuma wameacha moshi mkubwa na uharibifu, vifo, na juu ya yote, chuki... na mara nyingine hata vita vya wenyewe kwa wenyewe. Fikiria kama jeshi la Kenya lingekuwa na aina ya rasilimali fedha ambazo majeshi ya nchi za magharibi wanazo! Sambamba na sera yetu ya nje ya amani, jeshi la Kenya linaondoa tishio la Al-Shabab lakini wakati huo huo linawapa Wasomali wasio na hatia nafasi ya kuanza maisha yao upya na kujikusanya. Mwisho wa vita, sisi kama Wakenya bado tutakuwa na fahari kwa kuhusishwa na maendeleo na ustawi wa ndugu na dada zetu nchini Somalia. Idumu milele Kenya ... Viva majeshi ya Kenya popote mlipo. Tunaona fahari sana ya kile mnachofanya.

  • kevin getonto otwori
    June 23, 2012 @ 04:56:50AM

    Ninaipenda hiyo lakini tafadhalini mnapaswa kuwa na tahadhari msiwadhuru watu wasio na hatia kama watoto.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo