Juni 21, 2012
Idadi ya aina uadimufu ya pundamilia wajulikanao kama Grevy inapungua kwa sababu ya ugombaniaji wa maeneo ya kuchunga mifugo nchini Kenya, liliripoti shirika la habari la AFP hapo Alhamis (tarehe 21 Juni).
Kupotea kwa aina za viumbe hao kunakochangiwa na kuongezeka kwa idadi ya watu, uwindaji na maradhi kunamaanisha kwamba ni pundamilia wachache chini ya 2,500 waliobakia, ikilinganishwa na 15,000 waliokuwepo mwaka 1970.
Eneo la hifadhi ya wanyama la West Gate katika mbuga za Naibelibeli nchini Kenya lilikuwa nyumbani kwa aina ya pundamilia ya Grevy 500 wakati mmoja, lakini ziara ya karibuni ya wataalamu wa wanyamapori imegundua kwamba wamebakia watano tu. Pundamilia wa Grevy wanaotambuliwa kwa masikio yao marefu na michoro tofauti na pundamilia wa kawaida, walikuwa wakionekana katika maeneo ya Somalia, Djibouti, Eritrea, Kenya na Ethiopia, lakini sasa wanaonekana Kenya na Ethiopia tu.
“Watu wanajikalia na kujichungia wanyama kila mahala,” alisema Peter Lalampaa kutoka kabila la Samburu na meneja mwandamizi wa mfuko wa Pundamilia wa Grevy, ambaye aliitembelea hifadhi ya wanyama ya West Gate. “Shule zinajengwa kwa wingi hapa na wachungaji waliozoea kurandaranda sasa wamekaa mahala mamoja, kwa hivyo uchungaji wa papo kwa papo limekuwa tatizo.”
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
Mahakama moja ya Bosaso iliwatia hatiani na kuwapiga faini Wairani 78 siku ya Jumapili (tarehe 19...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata watuhumiwa 15 kuhusiana na kulichoma Kanisa la Bethania kweny...
Mkuu wa Polisi wa Kenya, David Kimaiyo, ameondoa nafasi za afisa polisi wa jimbo, afisa wa upelel...
Watu wenye silaha waliwaua watu wawili na kuwajeruhi wengine wanne katika mashambulizi tofauti kw...
Mkutano wa kuzungumzia uwezekano wa uchimbaji mafuta na gesi, uwekezaji, usalama na miundombinu n...
Wizara ya Masuala ya Wanawake na Familia ya Puntland ilianza mafunzo ya siku nane hapo Juampili (...
Zaidi ya Wasomali milioni 1 hawatakuwa na "usalama wa chakula" hadi mwezi wa Septemba, Mtandao wa...
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Nadhani hakuna maisha mazuri zaidi ya maisha ya utulivu na kazi itokanayo na kilimo, na tutafaidika sana ikiwa tutafanikiwa kuivutia jamii ya wafugaji kufanyakazi katika sekta ya kilimo na kulima mashamba na kufuga mifugo. Hili ndilo tunalotaka, kwa sababu hatua hii chanya itakua hatua kubwa kwa kiwango cha uchumi. Ili kufikia hatua hii, serikali lazima iwaunge mkono na kuiitia moyo sekta ya kilimo kwa kupeana mahitaji yote ya wakulima, na kuwafanya wajihisi kuwa inawashughulikia wao na ardhi yao na kwamba itawapatia mahitaji yanayohitajika na kununua mazao yao, pamoja na kushughulikia matatizo mengine ambayo sekta ya kilimo imeshuhudia hivi karibuni.
Mnahitajika kuweka picha katika machapisho yenu.