Juni 21, 2012
Makampuni kutoka Ufaransa yanajitayarisha kuwekeza nchini Tanzania, alisema mwanadiplomasia wa ngazi za juu wa Kifaransa hapo Jumanne (tarehe 19 Juni).
“Licha ya baadhi ya changamoto, uchumi wa Tanzania unakuwa…katika maeneo ya biashara, uwekezaji, na kadhalika.” Mkurugenzi Mkuu anayehusika na masuala ya Afrika wa Ufaransa Elisabeth Barbier aliliambia gazeti la The Guardian la Tanzania. "Makampuni ya Ufaransa yako tayari kuwekeza nchini Tanzania. Wanataka kunufaishwa na uwezo wa ukuaji na maendeleo uliopo."
Alisema uwezo wa kuwekeza nchini Tanzania unatakiwa kutumiwa vyema ili kutoa matokeo mazuri katika kiwango cha umma, kama vile kuinua hali ya maisha ya wananchi.
Barbier pia alibainisha kuwa Umoja wa nchi za Ulaya unampango kuwa mbia na Tanzania na nchi nyingine za Afrika ili kupambana na maharamia.
“Katika kiwango cha Umoja wa nchi za Ulaya kuna mradi maalum ambao utaanza hivi karibuni kujenga uwezo wa baadhi ya nchi za Afrika, Tanzania ikiwa mojawapo, kupambana na wimbi linaloongezeka la maharamia kwenye Bahari ya Hindi,” alisema.
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
Mahakama moja ya Bosaso iliwatia hatiani na kuwapiga faini Wairani 78 siku ya Jumapili (tarehe 19...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata watuhumiwa 15 kuhusiana na kulichoma Kanisa la Bethania kweny...
Mkuu wa Polisi wa Kenya, David Kimaiyo, ameondoa nafasi za afisa polisi wa jimbo, afisa wa upelel...
Watu wenye silaha waliwaua watu wawili na kuwajeruhi wengine wanne katika mashambulizi tofauti kw...
Mkutano wa kuzungumzia uwezekano wa uchimbaji mafuta na gesi, uwekezaji, usalama na miundombinu n...
Wizara ya Masuala ya Wanawake na Familia ya Puntland ilianza mafunzo ya siku nane hapo Juampili (...
Zaidi ya Wasomali milioni 1 hawatakuwa na "usalama wa chakula" hadi mwezi wa Septemba, Mtandao wa...
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji