Juni 21, 2012
Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) linaendelea kujitolea kuwasaidia wakimbizi wa Somalia, msemaji wa shirika hilo, Adrian Edwards, aliliambia gazeti la Kulmiye News la Somalia hapo Jumatano (tarehe 20 Juni).
Edwards alisema UNHCR inaendelea kuwahudumia wakimbizi wa Kisomali nchini Kenya, Uganda, Ethiopia, Djibouti na Misri.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, pia alisisitiza ulazima wa hali ya wakimbizi wa Somalia hapo Jumatano katika Siku ya Wakimbizi Duniani, akitaja kwamba makambi ya wakimbizi ya Dadaab ni mji wa tatu kwa ukubwa nchini Kenya ukiwahifadhi Wasomali 500,000. “Nchi zinazowahifadhi wakimbizi hazipaswi kuachiwa mzigo huu peke yao”, alisema.
“Ni lazima tufanye kazi pamoja kuhamasisha dhamira ya kisiasa na uongozi kuzuia na kumaliza migogoro inayopeleka wakimbizi kumiminika sehemu nyingine,” alisema Ban. “Pale usalama unaporudishwa, lazima tutatue mambo yanayosababisha migogoro, kuruhusu kurudi kwa wakimbizi nyumbani kupitia upatikanaji wa maisha, huduma, na utawala wa sheria.”
Wizara ya Usafiri wa Anga ya mkoa wa Somaliland siku ya Jumanne (tarehe 18 Juni) iliikataza ndege...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata makamu wanne wa chama kikuu cha upinzani cha Demokrasia na Ma...
Watu wenye silaha kwenye Kaunti ya Wajir walimuua polisi mmoja wa akiba wa Kenya siku ya Jumanne ...
Japan inaipa Tanzania dola milioni 49 (shilingi bilioni 80.4) kama msaada na mkopo kwa ajili ya k...
Inspekta Jenerali wa Polisi David Kimaiyo yeye pekee yake amewateua na kuwapangia kazi maafisa wa...
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) siku ya Jumanne ilimkubalia Makamu wa Rais wa Kenya Willia...
Polisi waliwakamata mamia ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa al-Shabaab katika wilaya za Hod...
Kongamano la siku tatu juu ya elimu lilifunguliwa mjini Mogadishu siku ya Jumanne (tarehe 18 Juni...
Wanajeshi wa serikali ya Somalia wakisaidiwa na wanajeshi wa Misheni wa Umoja wa Mataifa (AMISOM)...
Waziri wa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa, Joseph Ole Lenku, siku ya Jumatatu (t...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji