Juni 21, 2012
Kamati ya Bunge la Kenya lilisema shilingi bilioni 83.5 (dola bilioni 1) zilizotengwa kwa usalama katika bajeti ya mwaka 2012-2013 hazitoshi.
Fedha zilizotengwa kwa usalama wa taifa hazitoshi, kutokana na vitisho vingi vinavyoikabili nchi kwa sasa,” Fred Kapondi, mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya utawala na usalama wa taifa, alisema hapo Jumatano (tarehe 20 Juni) katika Redio Milele ya Kenya.
Ingawa serikali hapo Aprili ilitangaza mpango wa kuajiri maafisa wapya 7,000 kuelekea uchaguzi ujao, pesa zilizotolewa ni kwa maafisa 3,500 tu, gazeti la Daily Nation la Kenya liliripoti.
Ili kuongeza usalama, serikali inachukua hatua za kupunguza uwepo wa silaha za moto, ikiwa ni pamoja na kurekebisha Muswada wa Silaha za Moto ili kutoa adhabu kali kwa umiliki wake usio halali, gazeti la The Standard la Kenya liliripoti.
Ripoti ya Silaha Ndogondogo iliyotolewa Jumatano inasema kuna kiasi cha silaha za moto haramu 680,000 nchini Kenya.
"Silaha hizi zimetapakaa kila sehemu lakini tunatumaini kuchukua hatua za kukabiliana na usumbufu mbele ya uchaguzi," alisema Mutea Iringo Katiba wa Kudumu ya Wizara ya Usalama wa Ndani.
Iringo alisema mzozo na al-Shabaab nchini Somalia umezidisha kuenea kwa silaha haramu. “Tuna matumaini kuwa operesheni nchini Somalia italeta busara hatimaye kwa sababu huu ndio chanzo kikuu cha tatizo hili,” alisema.
Iwapo sheria zitarekebishwa, wamiliki wa bunduki haramu watafungwa kifungo cha maisha, ambapo adhabu kubwa kwa sasa nikifungo cha miaka 15, kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation.
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
Watu watano walikamatwa siku ya Jumanne mjini Dar es Salaam wakiwa na vifaa vya kulipua katika mi...
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliwataka wabunge kuweka kando madai yao ya kuongezwa mishahara kwa ...
Majeshi ya serikali ya Somalia waliwaua wanamgambo tisa wa al-Shabaab wakati wa mapambanao hapo J...
Mtu asiyejulikana alimpiga kwa risasi na kumuua ofisa wa kitengo cha usalama cha kijeshi huko kas...
Muungano wa Jubilee tawala cha Kenya kilichukua uongozi wa kamati mbili muhimu za bunge Ijumaa (t...
Chama cha Wafanyabiashara na Asasi ya Chakula na Kilimo ya Umoja wa Mataifa vinatoa mafunzo kwa w...
Balozi wa Umoja wa nchi za Ulaya nchini Tanzania Filiberto Ceriani Sebregondi aliwahamiza waandis...
Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, alisema kazi za Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji