Juni 21, 2012
Vikosi vya usalama vya Somalia vimewaokoa wanandoa kutoka Afrika ya Kusini ambao walitekwa nyara katika Bahari ya Hindi na kuzuiliwa kwa muda wa miezi 18, Waziri wa Ulinzi wa Somalia Hussein Arab Isse alisema hapo Alhamisi (tarehe 21 Juni).
“Uokozi ulianza usiku uliopita (wa Jumatano) na ulidumu mpaka asubuhi hii na mnaweza kuona kuwa wanandoa waliokolewa salama,” Isse alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na wanandoa hao, Debbie Calitz na Bruno Pelizzari.
Isse alisema uvamizi huo ulikuwa ni operesheni ya pamoja baina ya vikosi vya usalama na jeshi na kwamba wanandoa wamekomolewa kutoka kwa “waasi wenye uhusiano na al-Qaeda”, kwa mujibu wa AFP.
Calitz and Pelizzari walikuwa wakisafiri katika Bahari ya Hindi nje ya mwambao wa Kenya mwaka 2010 ambapo boti yao ya kifahari ilipotekwa nyara na maharamia 12 walioipelea Somalia na kuwachukua wanandoa huko Barawe.
Afrika ya Kusini ilikaribisha habari za kuokolewa kwa wanandoa hao na kuwashukuru watu wote waliohusika katika operesheni.
“Serikali ya Afrika ya Kusini inataka kuelezea shukurani zake za dhati kwa Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia kufuatia kwa kuachiwa huru kwao hapo Jumatano,” Waziri wa Mambo ya Nje alisema katika taarifa. “Wanandoa wako katika afya njema na wana hamu ya kuungana na wapendwa wao.”
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
Ukiritimba na ukosefu wa ufanisi katika bandari ya Dar es Salaam unaigharimu Tanzania na nchi jir...
Viongozi wa mkoa wa Puntland walikutana siku ya Jumanne (tarehe 21 Mei) kuwashajiisha wanawake ku...
Wanajeshi wa Somalia na wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) waliwakamata zaidi ...
Rais Ismail Omar Guelleh wa Djibouti alijadiliana ushirikiano wa kimkakati na Kanali Saleh Ben Na...
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, vikosi vya usalama na mahakama vinapaswa kuomba radhi hadharani kut...
Waziri Mkuu wa Djibouti Abdoulkader Kamil Mohamed alitoa wito wa kuongezwa kwa ushirikiano katika...
Baadhi ya wabunge wa Somalia wameitupilia mbali hoja ya kumtaka waziri mkuu na baraza lake la maw...
Wabunge wa upinzani walidai kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikibana uhuru wa kujieleza na kud...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Wanandoa hawa walikuwa sehemu ya mabaharia katika boti ya fahari iliyokuwa ikielekea Richards Bay Afrika ya Kusini - na ambayo ilitekwa nyara nje ya mwambo wa Tanzania. Hata hivyo kepteni wa Afrika ya Kusini wa boti ndogo aliokolewa na meli ya jeshi la majini la Uholanzi iliyokuwa inawafukuza maharamia wakati ule, na maharamia watano walikamatwa na kushitakiwa katika mahakama ya sheria ya Uholanzi, ambapo Waholanzi waliweza pia kumuokoa kepteni. Hata hivyo wanandoa hawa wa Africaans - ambao ni daraja la wafanyakazi masikini - walizuiwa kwa mtutu wa bunduki na maharamia waliobaki waliokuwa wakikimbia - kwa hivyo kushindwa kukimbia. Hii ilipelekea kukamatwa kwao. Shukrani nyingi kwa watu wa somalia kwa njia yao ya ubinadamu ya kushughulikia opresheni hii ya kuwaokoa wanandoa masikini kifedha ambao familia zao zilikuwa zikijaribu kwa kukata tamaa ili kukusanya fedha za kikomboleo.