Juni 20, 2012
Baraza la Mawaziri la Somalia lilifanya mkutano wiki hii kujadili vizuizi vya barabara visivyo halali ambavyo vimeanzishwa Mogadishu yote kwa miongo miwili iliyopita, Mtandao wa habari wa Shabelle wa Somalia uliripoti Jumanne (tarehe 19 Juni).
Waziri wa habari, Posta na Mawasiliano Abdulkadir Hussein Mohamed alisema baraza la mawaziri kwa pamoja lilikubaliana “kuchukua hatua kali dhidi ya vituo vya ukaguzi visivyo halali vinavyosumbua Mogadishu na vijiji vya jirani chini ya udhibiti wa Serikali ya Mpito ya Shirikisho.”
Waziri pia alisema Waziri Mkuu Abdiweli Mohammed Ali amekuwa akikutana na mashirika ya ulinzi ya taifa na wakazi wa Mogadishu kujadili vizuizi vya barabarani.
Waendesha pikipiki wamelalamika kwamba watu wenye silaha waliovaa sare za serikali wanadai fedha kwa nguvu katika vituo vya ukaguzi.
Vikosi vya serikali ya Somalia huko Mogadishu hivi karibuni vilirushiana risasi na watu wenye silaha waliovaa sare za jeshi, Shabelle iliripoti Jumanne.
Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Hodan Hassan Mohammed Abukar alisema mapigano yaliendelea baada ya vikosi vya ulinzi kuwavamia watu wenye silaha ambao walikuwa wakichukua fedha kinyume cha sheria katika kituo cha ukaguzi.
"Vikosi vya ulinzi vimemkamata mmoja wa genge la wahalifu wakati wa operesheni na kumkabidhi kwa mahakama ya kijeshi ya Somalia ili sheria ichukue mkondo wake kutokana na kujihusisha kwake katika kuwapora raia huko Mogadishu,” Abubakar alisema.
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
Mahakama moja ya Bosaso iliwatia hatiani na kuwapiga faini Wairani 78 siku ya Jumapili (tarehe 19...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata watuhumiwa 15 kuhusiana na kulichoma Kanisa la Bethania kweny...
Mkuu wa Polisi wa Kenya, David Kimaiyo, ameondoa nafasi za afisa polisi wa jimbo, afisa wa upelel...
Watu wenye silaha waliwaua watu wawili na kuwajeruhi wengine wanne katika mashambulizi tofauti kw...
Mkutano wa kuzungumzia uwezekano wa uchimbaji mafuta na gesi, uwekezaji, usalama na miundombinu n...
Wizara ya Masuala ya Wanawake na Familia ya Puntland ilianza mafunzo ya siku nane hapo Juampili (...
Zaidi ya Wasomali milioni 1 hawatakuwa na "usalama wa chakula" hadi mwezi wa Septemba, Mtandao wa...
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji