Umoja wa Mataifa waratibu semina ya Mogadishu kuhusu wanawake katika siasa

Juni 19, 2012

  • 1 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Ofisi ya Siasa ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Somalia imewezesha semina ya wanawake iliyohusu ushiriki katika siasa huko Mogadishu ambayo ilimalizika siku ya Jumatatu (tarehe 18 Juni), Redio Bar-Kulan inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa iliripoti.

Waziri wa Wanawake aliratibu semina hiyo ambayo wanawake 37 walijifunza njia za kuongeza wajibu wao katika siasa ya Somalia. Waziri Maryan Aweys alisema wanawake wa Somalia wanapaswa kutumia asilimia 30 ya fungu walilotengewa kwani Somalia imeshapita katika utawala wa mpito.

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Augustine Mahiga aliwahimiza wanawake kuzidisha jitihada zao mara mbili ili kutatua migogoro ya kisiasa nchini Somalia.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • abdi
    June 20, 2012 @ 01:56:38AM

    Kufanyika kwa mikutano ya kimataifa nchini Somalia ni faida kwa watu na uchumi wa Somalia. Mikutano ina dhamira ya kuonyesha kuwa Somalia ina mwanga tofauti na kuonyesha ulimwengu wote hatua kubwa ambazo nchi inapiga katika kuijenga upya nchi yao. Mikutano ya kimataifa ina umuhimu mwingine kwa nchi kwa sababu inasaidia kueleza baadhi ya masuala nyeti na kujaribu kuyatafutia suluhisho. Mkutano wa kimataifa vile vile unairuhusu serikali ya Somalia kuomba misaada zaidi ya wafadhili kutoka kwa jumuiya ya kimataifa. Umuhimu mkubwa wa mkutano wa kiamtaifa ni kuwakaribisha wawekezaji wa kigeni kuja na kuwekeza Somalia ambapo masoko yamekua kwa nguvu, Hili pia litasaidia kuionesha kile Somalia ilicho nacho kama vile utamaduni, fursa za kibiashara na mengine zaidi.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo