Juni 11, 2012
Vikosi vya Serikali ya Mpito ya Shirikisho na washirika wake vina mpango wa kuwamaliza al-Shabaab kabla ya tarehe ya mwisho ya serikali ya mpito mwezi Agosti, Waziri Mkuu wa Somalia Abdiweli Mohamed Ali alisema.
“Vikosi vya serikali ya Somalia, kwa msaada wa walinda amani wa Umoja wa Afrika, wanadhamiria kumaliza udhibiti wa al-Shabaab nchini Somalia,” Ali alisema kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Shabelle Media Network wa Somalia, uliripoti hapo Jumatatu (tarehe 11 Juni). “Al-Shabaab wamepoteza maeneo yao mengi sana ndani ya kipindi cha miezi 18 ya kushambuliwa kutoka majeshi ya Umoja wa Afrika, serikali ya Somalia, Ethiopia na Kenya.”
Vikosi vya Somalia na vya washirika wake vimeichukua mikoa muhimu katika maeneo ya kusini na kati ya Somalia, alisema Ali.
Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, alisema kazi za Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alipokea vyeti vya utambul...
Kwa uchache watu wanne waliuawa na watatu kujeruhiwa siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) baada ya wa...
Kenya na Tanzania zilifanya operesheni ya pamoja ya ulinzi wa mpaka siku ya Alhamisi (tarehe 16 M...
Mwanachama wa kundi la wanamgambo wanaoiunga mkono serikali ya Somalia la Ahlu Sunna wal Jamaa, A...
Wanawake watatu waliuawa usiku wa Alhamisi (tarehe 16 Mei) katika eneo la Malkamau kwenye Kaunti ...
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon. siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alimteua waziri wa...
Tanzania na Canada zimesaini mkataba wa ushirikiano yanayokusudiwa kuimarisha na kuunda mazingira...
Jeshi la Taifa la Somalia liliwauwa wanamgambo 13 wa al-Shabaab siku ya Jumanne (tarehe 14 Mei), ...
Muda wa mwisho kwa wakaazi wa Mandera kusalimisha silaha zao haramu umeongezwa hadi Ijumaa (tareh...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Mungu awalaani magaidi wote wanaojaribu kufanya mashambulizi maovu ya kigaidi, wakikusudia kupandikiza hofu na kueneza vurugu na uhalifu; pamoja na kuchochea migogoro. Tayari wamesababisha vifo vya watu wengi wasio na hatia kwa kupiga mabomu ya kutega, kuua, kuteka nyara na kuchinja, kuiba na kutesa na kuendeleza mfululizo wa ukiukaji wa haki dhidi ya raia wasio na hatia. Watu hawa ni vikundi vya kigaidi tu, vinavyohakikisha kujilimbikizia mali wakati vinahatarisha usalama na utulivu wa taifa. Lengo lao ni kuigeuza Somalia kuwa taifa la fujo na lisilo na utulivu, kuondosha amani na utulivu. Kwa hivyo, Mungu amlaani kila mtu anayesababisha madhara, uharibifu, ugaidi na maovu kwa watu. Tunamuomba Mungu kumuokoa kila mtu kutokana na maovu na madhara yao, na kurejesha usalama wa nchi. Tunamuomba Mungu kuleta ahuweni kwa nchi zote zinazoteseka kutokana na tatizo kama hili. Kila mtu sasa anahisi shinikizo la vurugu na ugaidi unaosababishwa na wahalifu na magenge haya. Wanajaribu kuwadhibiti watu kwa nguvu. Wanatumia fursa ya hali mbaya ya nchi, kujenga uwepo wao miongoni mwa watu na baadaye kufanya ugaidi na kuwatisha. Wanataka kupandikiza hofu, mfumo wa vikundi vya imani, chuki, uhasama na mapigano miongoni mwa watu, ili fujo zienee kila pahali.
Somalia inacho kikundi cha kigaidi hatari sana katika Afrika, Al-Shabaab na uhalifu wao wa kutisha kwa binadamu na uharibifu wa mali. Uhalifu wa kwanza ambao kikundi hiki kinahusika nao ni kuandikisha watoto kama askari. Wanawateka nyara watoto wadogo na kuwatumia kama askari na kusema kwamba watoto ni rahisi kuwafinyanga. Al-Shabaab pia wanahusika na mauaji ya watu wasio na hatia katika vita vyao dhidi ya serikali ya shirikisho nchini Somalia. Vile vile, al-Shabaab wanahusika na vitendo vya uhalifu katika nchi jirani kama vile Kenya na Ethiopia. Uhalifu huu ni mbaya kwa watu wa Somalia na kwa bara la Afrika kwa ujumla kwa sababu zinawakimbiza wawekezaji wa kigani na matokeo yake ni kuathiri uchumi wa bara la Afrika.