Ufaransa yaikopesha Kenya dola milioni 98.1 kujenga laini za umeme

Juni 10, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Serikali ya Kenya imetilaiana saini na Shirika la Maendeleo la Ufaransa makubaliano ya mkopo wa shilingi bilioni 8.3 (dola milioni 98.1), radio ya Kenya Capital FM News iliripoti hapo Ijumaa (tarehe 8 Juni).

Fedha hizo zitapelekwa katika ujenzi wa laini la kutolea umeme wa volteji kubwa katika eneo kubwa la Nairobi. Waziri wa Fedha Njeru Githae alisema mradi huo utatoa uwezo wa ziada wa usambazaji umeme kutoka viwanda vipya vya umeme wa ardhini katika Olkaria na kiwanda kipya cha umeme wa upepo kitakachojengwa karibunikatika ZiwaTurkana.

Waziri Njeru Githae alisema mradi huo utasaidia kiwango cha mahitaji kinachoongezeka cha umeme. “Tunataka kuhakikisha kuwa watoto wetu watakaozaliwa miaka miwili kutoka sasa kuwa katika maisha yao, neno “giza tupu” wawe hawalijui,” alisema.

Balozi wa Ufaransa Etienne de Poncins alisema hii ni ya kipaumbele kwa maendeleo mijini na ya kitaifa, ikiwa na uwezo wa kuwa na athari za muda mrefu.

“Mpango huu utasaidia kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi mjini Nairobi na nchini kote kwa jumla kwa kuwa na umeme wa kutosha kwa madhumuni ya kiusalama,” alisema. “Kwa muda mrefu, tunataka kujishughulisha na mradi wa kuuanganisha umeme na Ethiopia na Tanzania chini ya Ubia wa Umeme wa Afrika ya Mashariki.”

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo