Juni 10, 2012
Waziri wa Mambo ya ndani wa Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Abdisalam Moallin Mohamud aliahidi katika mkutano wa hadhara hapo Jumapili (tarehe 10 Juni) kuwa amani itarejea Mogadishu, Mtandao wa habari wa Somalia wa Shabelle News uliripoti.
Akizungumza kwenye sherehe katika wilaya ya Howlwadaag ya Mogadishu, Mohamud alisema mipango iko njiani ya kuimarisha usalama, sheria na kanuni mjini.
“Ninawaomba watu wa Mogadishu kushirikiana pamoja na kuvisaidia vikosi vya usalama vya serikali ya Somalia kudhibiti usalama kwa jumla jijini ili kuzuwia mashambulizi na mauaji dhidi ya raia,” alisema.
Mwezi uliopita, mfulizo wa milipuko jijini iliua kiasi cha watu saba, wengi wao wakiwa askari. Wiki iliyopita watu wenye silaha walimuua mfanyabiashara mmoja wa Uturuki.
Mogadishu imekuwa katika udhibiti wa Serikali ya Mpito ya Shirikisho tangu al-Shabaab walipolazimishwa kuondoka mwezi Agosti 2011.
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
Watu watano walikamatwa siku ya Jumanne mjini Dar es Salaam wakiwa na vifaa vya kulipua katika mi...
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliwataka wabunge kuweka kando madai yao ya kuongezwa mishahara kwa ...
Majeshi ya serikali ya Somalia waliwaua wanamgambo tisa wa al-Shabaab wakati wa mapambanao hapo J...
Mtu asiyejulikana alimpiga kwa risasi na kumuua ofisa wa kitengo cha usalama cha kijeshi huko kas...
Muungano wa Jubilee tawala cha Kenya kilichukua uongozi wa kamati mbili muhimu za bunge Ijumaa (t...
Chama cha Wafanyabiashara na Asasi ya Chakula na Kilimo ya Umoja wa Mataifa vinatoa mafunzo kwa w...
Balozi wa Umoja wa nchi za Ulaya nchini Tanzania Filiberto Ceriani Sebregondi aliwahamiza waandis...
Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, alisema kazi za Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Asanteni sana majeshi ya AMISOM (UA) kwa kazi mliyofanya; baada ya miaka 20 Somalia amani inaweza kurejeshwa sasa, na kwa kweli mnastahiki sifa kwa hilo. Maisha marefu AMISOM, maisha marefu kwa UA. Kwa upande wangu, sitaki mazungumzo ya amani na al-Shabaab kwa sababu wameshaona baada ya kushindwa ndio wanataka mazungumzo, hapana. AMISOM endeleeni na kuwafunza nidhamu al-Shabaab bila ya huruma.