Juni 10, 2012
Waandishi wa habari na vikundi vya vyombo vya habari vimelaani mauaji yanayolengwa waandishi wa habari baada ya watu wenye silaha kumpiga risasi na kumjeruhi mtoa habari wa radio Mohamed Nur Sharif siku ya Ijumaa jioni (tarehe 8 Juni).
Sharif, anayefanyakazi katika Radio Bar-Kulan inayofadhiliwa na UN, alipigwa risasi alipokuwa akirejea nyumbani kutoka mitaa ya Hamar Jajab mjini Mogadishu. Watu watatu waliokuwa na bastola walimpiga risasi Sharif mara mbili, moja ya kifua nyengine ya mgongo, Bar-Kulan iliripoti.
Sharif alifanyiwa upasuaji anaendelea vizuri. Hii ni mara ya pili kwa Sharif kujeruhiwa akiwa kazini. Mwezzi wa Aprili, alikuwa miongoni mwa waandishi wa habari zaidi ya kumi waliojeruhiwa katika bomu la kujitoa muhanga la al-ShabaaJumba la Taifa la Maonesho
"Tunalaani mashambulizi haya ya kutisha dhidi ya wenzetu wakati washambuliaji hao hawaadhibiwi,” alisema Katibu Mkuu wa Umoja wa Kitaifa wa Waandishi wa Habari wa Somalia Mohamed Ibrahim. “Tunaitaka serikali ya Somalia kufanya uchunguzi huru mara moja kuhusu tukio hili.”
Jumuiya ya Waandishi wa Habari wa Somalia walioko Uhamishoni huko Nairobi (SEJASS) pia walilaani jaribio hilo la mauaji na kuitaka serikali ya Somalia “ kufanya uchunguzi wa kina wa kesi hii na kuwakamata washambuliaji waliohusika”.
“Mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari kunahatarisha uhuru wa vyombo vya habari nchini,” mwenyekiti wa SEJAS Mohamed Osman Hussein alisema katika taarifa.
Hakuna kikundi kilichodai kuhusika na shambulio hilo. Mpaka sasa, waandishi wa habari watano wa Somali wameshauliwa mwaka huu na watu wenye silaha wasiojulikana.
Wizara ya Usafiri wa Anga ya mkoa wa Somaliland siku ya Jumanne (tarehe 18 Juni) iliikataza ndege...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata makamu wanne wa chama kikuu cha upinzani cha Demokrasia na Ma...
Watu wenye silaha kwenye Kaunti ya Wajir walimuua polisi mmoja wa akiba wa Kenya siku ya Jumanne ...
Japan inaipa Tanzania dola milioni 49 (shilingi bilioni 80.4) kama msaada na mkopo kwa ajili ya k...
Inspekta Jenerali wa Polisi David Kimaiyo yeye pekee yake amewateua na kuwapangia kazi maafisa wa...
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) siku ya Jumanne ilimkubalia Makamu wa Rais wa Kenya Willia...
Polisi waliwakamata mamia ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa al-Shabaab katika wilaya za Hod...
Kongamano la siku tatu juu ya elimu lilifunguliwa mjini Mogadishu siku ya Jumanne (tarehe 18 Juni...
Wanajeshi wa serikali ya Somalia wakisaidiwa na wanajeshi wa Misheni wa Umoja wa Mataifa (AMISOM)...
Waziri wa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa, Joseph Ole Lenku, siku ya Jumatatu (t...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Kuna habari gani za karibuni kutoka Somalia?
Al-Shabaab waelewe kuwa wanajichimbia kaburi lao wenyewe. Wanajisafishia njia ya kujimaliza wenyewe kwa kuua watu wasio na hatia.