Waziri wa Usalama wa Kenya afariki dunia katika ajali ya kuanguka kwa helkopta

Juni 10, 2012

  • 3 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya George Saitoti (kulia) akizungumza na Katibu Mkuu wa UN BanKi-moon katika Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi mwezi Machi 2011. [Simon Maina/AFP]

  • Waziri wa Usalama wa Kenya George Saitoti (kulia) akizungumza na Katibu Mkuu wa UN BanKi-moon katika Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi mwezi Machi 2011. [Simon Maina/AFP]

    Waziri wa Usalama wa Kenya George Saitoti (kulia) akizungumza na Katibu Mkuu wa UN BanKi-moon katika Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi mwezi Machi 2011. [Simon Maina/AFP]

Saitoti, mwenye umri wa miaka 66, alikuwa mgombea wa urais katika uchaguzi ujao na mtu muhimu katika kuendesha mapambano ya Kenya dhidi ya kikundi cha al-Shabaab wanaoshirika na al-Qaida katika nchi jirani ya Somalia. AFP iliripoti.

Helkopta hiyo ilidondoka katika msitu wa Kibuku kama saa 2:30 hivi asubuhi, muda mfupi tu baada ya kunyanyuka kutoka uwanja wa ndege wa Wilson wa Nairobi. Ilikuwa ikielekea kwenye sherehe za kidini huko magharibi mwa Kenya. Manahodha wawili na mabodigadi wawili pia walifariki katika ajali hiyo ya kuanguka kwa helkopta.

Rais Mwai Kibaki alisema katika taarifa kuwa vifo hivyo ni pigo kubwa kwa nchi yetu”.

"Waziri Saitoti atakumbukwa siku zote kwa kuwa alikuwa mchapakazi na aliyetumikia utumishi wa umma akitumia muda wake kuhudumia watu wa Kenya,” Kibaki alisema.

“Serikali itahakikisha uchunguzi wa kina wa ajali hiyo” kilichosababisha kuanguka . Waziri Mkuu Raila Odinga aliwaambia waandishi wa habari katika eneo la tukio.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 2)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • Dr Matthew Mwangi Theuri
    June 21, 2012 @ 11:41:09AM

    George Saitoti alikuwa mtu mkubwa, Daima atakumbukwa kwa msimamo wake thabiti dhidi ya utawala wa kidikteta wa Moi . Huko Kasarani na mbele ya Raisi Moi mtu huyu mzuri alisema, "zinakuja nyakati ambazo taifa litakuwa kubwa kuliko mtu binafsi." Huyu ndiye mtu ambaye alipaswa kuwa raisi wa nne wa jamhuri ya kenya. Roho yake na ya Msaidizi wake Ojodehh na wanne wengine ambao walikufa pamoja naye zipumzike katika amani ya milele. Dr Theuri Matthew Mwangi.

  • JOHN MWANGI
    June 11, 2012 @ 07:14:59AM

    Ilikuwa inashitusha kupòkea habari mbaya kama hizo. hata hivyo hakuna tunachoweza kufanya isipokuwa kukubali kuwa tumepoteza. Ningependa tu kuwafariji wanafamilia na marafiki zake. Tumuombe Mungu awape amnai katika wakati huu mgumu. Wote wawili Mungu awalaze pema - Amen.

  • ELIJAH NYABOGA
    June 11, 2012 @ 03:09:37AM

    Waziri wa Usalama wa ndani Professor Goerge angekuwa Raisi ajaye wa Kenya siku za mbele kwa mujibu wa uchambuzi wangu. Daima hakuwakandamiza wanasiasa wengine. Alikuwa rafiki wa jumuiya ya Kisii pamoja na Kenya kwa jumla. Mungu ibariki familia yake.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo