Maharamia wa Somalia waliachia huru meli na mabaharia baada ya miezi 7

Juni 08, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Maharamia wa Somalia waliiachia huru meli ya mafuta na kemikali inayomilikiwa na Ugiriki ikiwa na mabaharia 21 wa Ufilipini baada ya zaidi ya miezi saba ya kuihikilia, gazeti la Ufilipino la SunStar liliripoti.

Msemaji wa Idara ya Mambo ya Nje ya Ufilipini Raul Hernandez alisema Ijumaa (tarehe 8 Juni) kuwa meli ya MT Liquid Velvet iliachiwa huru hapo Jumatatu baada ya kushikiliwa tangu tarehe 31 Oktoba 2011.

Kwa sasa meli hiyo inasafiri kuelekea bandari ya Omani ya Salalah. Hakukuwa na ripoti ya mara moja iliyotolewa kuhusu fedha ya kukombolea meli hiyo.

Maharamia wa Somalia bado wanashikilia mateka mabaharia 45 katika meli tano huko Ghuba ya Adeni, gazeti liliripoti.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 4)

Dislike_icon(3)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, serikali za majimbo ya shirikisho ziundwe vipi nchini Somalia kufuatia utata wa Jubbaland?

Angalia matokeo