AMISOM, Vikosi vya AMISOM na Somalia vyatangaza shambulizi jengine dhidi ya al-Shabaab

Juni 08, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Vikosi vya usalama vya Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia na Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia (TFG) vinatayarisha mashambulizi dhidi ya al-Shabaab katika mji wa Balad, ulioko kilomita 30 kaskazini ya Mogadishu, kwa mujibu wa Jenerali Ugadi Kiki wa AMISOM.

"Baada ya kuhakikiha uaalama katika ushoroba wa Afgoye, uliojazana watu wa ndani waliokimbia makazi yao. Tunatayariha hambulizi jengine kubwa dhidi ya wanamgambo waliobakia katika eneo la Shabelle ya Chini,” Kiki aliema, mtandao wa Shabelle Media Network uliripoti hapo Ijumaa (tarehe 8 Juni). “Hii ni hatua yetu inayofuata ya Opereheni Yetu Shabelle Huru.”

Katika habari zinazohusiana na hizi, Waziri wa Ulinzi wa Somalia Hussein Arab Isse aliliambia baraza la mawaziri kuwa vikosi vya AMISOM na TFG vimefanikiwa kuviteka vijiji vingi na vinaendelea kuelekea katika mji wa Kismayo unaodhibitiwa na al-Shabaab, mtandao wa Shabelle Media Network uliripoti hapo Ijumaa.

Isse alisema pia kutakuweko na mahakama ya kijeshi huko Afgoye, ambako mtu yeyote katika jeshi atakayefanya uhalifu dhidi ya watu atahukumiwa.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 4)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, katiba ya Kenya inapaswa kurekebishwa ili kulipa baraza jipya la Seneti madaraka zaidi?

Angalia matokeo