Juni 08, 2012
Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia (TFG) hapo Ijumaa (tarehe 8 Juni) ilikaribisha zawadi ya mamilioni ya dola kama zawadi kwa habari zitakazopelekea kukamatwa kwa viongozi wa al-Shabaab.
“Tangazo kutoka serikali ya Marekani leo kuweka zawadi ya dau la dola milioni 7 kwa kiongozi wa kigaidi wa al-Shabaab bila shaka kutasaidia juhudi za serikali ya Somalia za kumaliza utawala wa vitisho wa al-Qaeda nchini Somalia,” TFG ilisema katika taarifa.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani iliwaongeza viongozi saba juu wa kikundi cha al-Shabaab chenye mafungamano na al-Qaeda kwa mpango wake wa Zawadi kwa ajili ya Haki hapo Alhamis.
Kiwango cha juu kabisa kilitolewa kwa muanzishaji wa kikundi, Ahmed Abdi aw-Mohamed, anayejulikana pia kama Ahmed Godane au Mukhtar Abu al-Zubair, kwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kutoa zawadi ya dola milioni za zawadi kwa habari za kujua alipo.
TFG ilisema Godane ni “dhamana wa mauaji ya wananchi wasio na hatia nchini Somalia, ikiwa ni pamoja na mfululizo wa mashambulizi ya kigaidi ambayo al-Shabaab wanafanya katika nchi za jirani.”
Dola nyingine milioni 5 zilitolewa kwa wanachama wengine wa al-Shabaab -- Ibrahim Haji Jama, Fuad Mohamed Khalaf, Bashir Mohamed Mahamoud na Mukhtar Robow.
Mpaka dola milioni 3 zilitolewa kwa Zakariya Ismail Ahmed Hersi na Abdullahi Yare.
“Hiki ni hali muhimu sana katika historia ya Somalia, ambapo uwezekano wa kupatikana tena nafuu upo karibu baada ya miaka mingi ya machafuko,” taarifa ilisema. “Serikali ya Somalia inatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuendelea kuzisaidia asasi ili kuhakikisha kuwa Somalia inashinda vita dhidi ya al-Qaeda, ambao wanashindwa kwa msaada wa watu wa Somalia.”
Uongozi wa Ahlu Sunna wal Jamaa katikati ya Somalia pia ulikaribia dau hilo la Marekani, na kuliita kuwa ni hatua moja mbele katika vita dhidi ya al-Shabaab, iliripoti Redio Bar-Kulan inayofadhiliwa na Umoja wa Matiafa.
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
Ukiritimba na ukosefu wa ufanisi katika bandari ya Dar es Salaam unaigharimu Tanzania na nchi jir...
Viongozi wa mkoa wa Puntland walikutana siku ya Jumanne (tarehe 21 Mei) kuwashajiisha wanawake ku...
Wanajeshi wa Somalia na wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) waliwakamata zaidi ...
Rais Ismail Omar Guelleh wa Djibouti alijadiliana ushirikiano wa kimkakati na Kanali Saleh Ben Na...
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, vikosi vya usalama na mahakama vinapaswa kuomba radhi hadharani kut...
Waziri Mkuu wa Djibouti Abdoulkader Kamil Mohamed alitoa wito wa kuongezwa kwa ushirikiano katika...
Baadhi ya wabunge wa Somalia wameitupilia mbali hoja ya kumtaka waziri mkuu na baraza lake la maw...
Wabunge wa upinzani walidai kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikibana uhuru wa kujieleza na kud...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Vikundi vya kigaidi vimepoteza wafuasi wao kwa sababu walikamatwa au kuuliwa wakati wa mapambano yaliyopinga vikosi vya usalama. Hii ndio sababu siku zote wanaandikisha wanachama wapya ili kuua watu wasio na hatia. Kwa hivyo, vyombo vya habari vinapaswa kufahamu wajibu wao, katika kuwaamsha vijana dhidi ya mbinu zao za kuwavutia. Pia mashule na vyuo vikuu vina nafasi muhimu, pamoja na misikiti na viongozi wa jamii ambao wana wajibu katika jamii ya Iraki. Wanapaswa kwenda mara moja, kuzuia uandikishwaji na kuwarubuni vijana. Kufanya hivi kutarejesha nyuma ugaidi. Watoto wetu wakiungana nao, majaliwa yao yatakuwa ni kifo katika mikono ya watu hawa wabaya na wahalifu; wanawatumia watoto wetu kwa kuwajaribu kwa pesa na madawa ya kulevya, au kuwadanganya kwa kutumia dini na kudai kuwa wanalinda watu na kwamba wako dhidi ya ugaidi. Kwa kweli, ni waongo, walaghai na wanavunja moyo; kwa hivyo hali halisi ya wahalifu na watu wabayahawa lazima ielezwe wazi.