Rais wa Somalia, wazee wajadili kuhusu Bunge la Katiba la Taifa.

Juni 07, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed alikutana na wazee wa kikabila Jumatano (tarehe 6 Juni) kujadili kuhusu uchaguzi wa wajumbe ambao wataidhinisha rasimu ya katiba.

Rais na Naibu Waziri wa Biashara Abdiwahab Ugas Hussein walikutana na wazee wa kikabila katika uwanja wa ndege wa Mogadishu kwa maombi ya wazee hao, Shirika la Habari la Taifa la Somalia liliripoti.

Ahmed alitoa wito kwa wazee hao kuitisha kamati yao iliyoanzishwa upya na kuchagua wajumbe wasomi kwa ajili ya Bunge la Katiba la Taifa kupiga kura kuhusu rasimu ya katiba. Uchaguzi wao unatakiwa uwe umekamilika ifikapo tarehe 20 Juni.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 1)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo