Polisi wa Kenya wawahoji watuhumiwa wa ugaidi

Juni 05, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Watu saba wahojiwa Jumatatu (tarehe 4 Juni) na Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Ugaidi Kenya kwa siku ya tatu mfululizo, baada ya kukamatwa Jumamosi kwa kuipiga picha ndege katika Uwanja wa Ndege wa Wilson, Nairobi.

Polisi wanawahoji watuhumiwa kujua nia yao ya kuipiga picha ndege, kaimu kamanda mkuu wa polisi Moses Ombati alisema, kwa mujibu wa Africa Review.

Sheria ya Kenya inaeleza kwamba watuhumiwa wanapaswa kupelekwa mahakamani ndani ya saa 24 baada ya kukamatwa kwao, lakini polisi hawajasema kwa nini wamewashikilia kwa muda mrefu bila ya kuwashitaki.

Kati ya watuhumiwa hao, wawili ni kutoka Somalia. Polisi ilisema wanadai kuwa wao ni watalii wanaopigapicha za wanyama nchini, ingawa simu zao za mkononi zilikuwa na picha ya ndege na uwanja wa ndege.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo