Bomu la kando ya barabara laua 6 huko Galkayo

Mei 31, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Si chini ya watu 6, wakiwemo raia watatu, waliuawa hapo Jumatano (tarehe 30 mei) kaskazini mwa eneo la Galkayo kutokana na bomu lililotegwa kando ya barabara kulipuka wakati vikosi vya usalama vilipokuwa vikijaribu kulitegua, AFP iliripoti.

"Watu watatu wa vikosi vya usalama na raia watatu waliuawa katika mlipuko huo, alisema afisa usalama Mahdi Abdulahi.

"Raia walidhani kuwa ilikuwa salama na wakasogea, lakini lililipuka," alisema Jama Alale, mwenye duka anayeishi jirani, na kuongeza kuwa aliona miili ya maiti huku viungo vyao vikiwa vimekatika kutokana na mlipuko huo.

Hakuna kikundi kilichodai kuhusika na mlipuko huo.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 1)

Dislike_icon(1)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, serikali za majimbo ya shirikisho ziundwe vipi nchini Somalia kufuatia utata wa Jubbaland?

Angalia matokeo