Jeshi la Kenya latabiri kuiteka Kismayo ifikapo Agosti

Mei 31, 2012

  • 3 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Mkuu wa jeshi la Kenya hapo Jumatano (tarehe 30 Mei) alisema kwamba AMISOM itauteka mji wa bandari wa Kismayo unaodhibitiwa na al-Shabaab ndani ya miezi mitatu.

Mji wa bandari wa Kismayo ni mji wa mwisho muhimu unaodhibitiwa na washirika wa al-Qaeda, al-Shabaaab, ambao katika miezi ya hivi karibuni wameanza kutumia mbinu za vita vya msituni wakati vikosi vya kanda vinaendelea kuwanyang'anya maeneo.

“Shabaha yetu hii itatokea kabla ya mwezi Agosti wakati utawala wa Serikali ya Mpito ya Shirikisho itakapomaliza muda wake,"alisema Jenerali Julius Karangi mjini Nairobi, kwa mujibu wa AFP. Vikosi kutoka Jeshi la Ulinzi la Kenya kwa sasa linafanya shughuli zake chini ya usimamizi wa AMISOM.

“Tunaendelea kutoa shinikizo kwa al-Shabaab,” Karangi alisema.

Wakati huo huo, majeshi ya Kenya yaliingia mji wa kusini ya Somalia wa Afmadow hapo Jumatano.

"Mji wa Afmadow unaanguka; bado kuna mapigano, lakini mpaka kumepambazuka utakuwa wetu,” alisema msemaji wa jeshi la Kenya Kanali Cyrus Oguna.

Wapiganaji wa al-Shabaab huko Afmadow, ambayo iko umbali wa kilomita 120 ndani ya Somalia kutoka mpaka wa Kenya, walizuia mashambulizi ya majeshi ya Kenya kwa miezi kadhaa, na kuyazuia yasisonge mbele kuelekea Kismayo.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 14)

Dislike_icon(4)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • somalifree
    July 3, 2012 @ 08:58:21AM

    Mimi si Muislamu, lakini furaha yangu ni ulimqengu wote kuishi kwa amani. Hakuna mtu atakayemuua mwengine kwa jina la dini, kwa sababu hayo si maumbile. Maumbile na Dini vinapaswa kukaa pamoja kwa dhamiri moja, kwa sababu kile kilicho kizuri hakihitaji kuelezwa. Somalia lazima iwe huru hatimaye kutoka mikono ya wahalifu hawa.

  • Dorine
    June 24, 2012 @ 05:55:48AM

    Maombi yetu sio kwa watu wetu tu bali pia kwa watu wa Somalia ambao wanashiriki katika kukombolewa kwa nchi. Mungu atapigana kwa ajili yenu. Ushindi utakuwa wenu.

  • susan
    June 1, 2012 @ 04:49:30PM

    Hilo litakuwa jambo zuri na tunawatakia kila la heri katika shughuli zenu zote. Mwenyezi Mungu awaongoze kama alivyomuongoza Daudu alipopambana dhidi ya Goliath.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo