Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kupeleka waangalizi wa uchaguzi nchini Kenya

Mei 31, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Uendeshaji wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) inajitayarisha kutuma timu ya Waangalizi ili kusimamia Uchaguzi Mkuu wa Kenya mapema mwaka 2013, mkuu wa EAC alisema siku ya Jumatano (tarehe 30 Mei).

“Tumealikwa na tume ya uchaguzi ya Kenya na kuchukua dhamana ya kuhakikisha kuwa waangalizi wanatumwa mapema kabla ya uchaguzi huo ili waweze kusimamia upigaji kura katika matayarisho ya mapema na kutoa ushauri unaofaa,” alisema Katibu Mkuu wa EAC Richard Sezibera wa Kongamano Dogo la VII juu ya Uongozi Bora Afrika mjini Arusha, kwa mujibu wa gazeti la Daily News la Tanzania.

Sezibera alisema kuwa nchi wanachama wa EAC zimekuwa zikisimamia vibaya uchaguzi wake wakuu, ambapo EAC inakusudia kufanya mabadiliko. Alisema kuwa viongozi wamekuwa wakijifanya wako juu ya sheria, na EAC inafanyakazi kuziba mapungufu hayo, kuzuia ufanyaji hila katika uchaguzi.

Nchi washiriki wa EAC ni pamoja na Kenya, Uganda, Rwanda, Tanzania na Burundi.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo