Mei 31, 2012
Wawakilishi kutoka nchi 54 walikusanyika mjini Istanbul hapo Alhamisi (tarehe 31 Mei) ili kutafuta njia kwa ajili ya hatma bora ya Somalia, AFP iliripoti.
Somalia inahitaji juhudi za kimataifa za ujenzi mpya ili kusaidia juhudi za sasa za utulivu na kusitisha miaka 20 ya machafuko katika Pembe ya Afrika, viongozi walisema katika ufunguzi wa Mkutano wa Pili Juu ya Somalia Mjini Istanbul.
Waziri Mkuu wa Somalia Abdiweli Mohamed Ali alisema Somalia iko tayari kwa maendelo ya muda mrefu na kuwaomba “wafadhili wengi kutoa mchango wa amana kwa Somalia”.
“Hatima ya Somalia iko mikononi mwa Somalia,” alisema katika ufunguzi wa mkutano wa siku mbili.
Naibu Waziri Mkuu wa Uturuki Bekir Bozdag alisema, “Baada ya kipindi kirefu cha kutokuwepo kwa utulivu na mgogoro, sasa mbele yetu tuna fursa kwa amani na usalama wa kweli.”
Bozdag alisema Mogadishu iko wazi kwa biashara na kutoa wito wa juhudi za kimataifa za ujenzi mpya.
"Tupo katika kilele cha uwezekano wa mabadiliko ya bahari, na Somalia inayo fursa nzuri ya amani kwa miongo kadhaa sasa,” alisema Mwakilishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Augustine Mahiga, na kutaja ushindi wa kijeshi dhidi ya al-Shabaab na “kushamiri” kwa biashara mjini Mogadishu. “Ni matumaini yangu kuwa mkusanyiko huu utafafanua mambo ya mikakati baada ya Agosti, na kuimarisha umiliki wa Somalia wa mchakato katika ubia na watendaji wa kikanda na kimataifa.”
Mkutano huo wa siku mbili – unaofuatiwa na Mkutano wa London hapo Februari -- ulianza kwa majadiliano miongoni mwa maafisa waandamizi, wataalamu na wafanyabiashara juu ya masuala manne makuu: maji, nishati, barabara na uendelevu.
Siku ya Ijumaa, mkutano utashughulikia upeo wa sera ya msaada kwa Somalia, kwa ushiriki wa mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, Rais wa Somalia Sharif Sheikh Ahmed, Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza William Hague.
Lengo moja kuu la mkutano hilo litakuwa kueleza kwa muhtasari hatima ya Somalia kwa kupanga malengo hadi 2015, kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje wa Uturuki.
Mamlaka ya serikali ya mpito ya Somalia yatamalizika mwezi Agosti. Viongozi wa Somalia hivi karibuni walikubaliana juu ya ratiba kwa urefu ambayo itaonesha hatua zinazohitajika ili kumaliza kipindi cha mpito na kuchagua raisi mpya.
Baadhi ya wabunge wa Somalia wameitupilia mbali hoja ya kumtaka waziri mkuu na baraza lake la maw...
Wabunge wa upinzani walidai kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikibana uhuru wa kujieleza na kud...
Sampuli ya DNA iliyochukuliwa kwenye mswaki uliokuwemo kwenye begi lililokuwa na risasi lililopat...
Wakenya kumi na wasaba wameshtakiwa kwa kuvunja amani, kufanya ghasia na ukatili dhidi ya wanyama...
Al-Shabaab imedai kuhusika na urushwaji wa makombora kwenye kasri ya rais mjini Mogadishu siku ya...
Wanajeshi wa Uganda wa Kikosi Namba 9+ wanarudi nyumbani baada ya kukamilisha miezi 13 ya ziara y...
Kikosi cha polisi cha Kenya kitaanza uhakiki wa kina wa maofisa mwezi ujao, kikianza na kusaili w...
Ujambazi ulizuiwa katika ofisi za usalama za Wells Fargo huko Mombasa ulisababisha kifo cha watu ...
Rais wa Ghana John Dramani Mahama aliahidi msaada wa nchi yake katika kipindi cha ujenzi mpya wa ...
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Baada ya kuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miongo miwili, Somalia imepata wakati wake kwa hivyo lazima waushikilie. Ni bahati nzuri pia kuwa ulimwengu unaelekeza macho yake kwa Somalia baada ya kuidharau kwa muda mrefu. Kwa hivyo hii ni fursa nzuri kwa ulimwengu wote kuiunga mkono kwani Somalia inauhitaji msaada huo.