Mamia ya watuhumiwa wa al-Shabaab wakamatwa huko Afgoye

Mei 29, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Vikosi vya Serikali ya Mpito ya Shirikisho na askari wa Umoja wa Afrika waliwakamata takriban watu 400 wanaotuhumiwa kuwa na uhusiano na al-Shabaab huko Afgoye siku ya Jumatatu (tarehe 28 Mei), Redio Bar-Kulan inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa iliripoti.

Ukamatwaji huo ulitokea wakati usafisha wa usalama wa mji wa Afgoye, ambao ulikombolewa kutoka kwa al-Shabaab wiki iliyopita. Operesheni hiyo iliongozwa na Jenerali Abdikhadir Sheikh Ali Dini, mkuu wa jeshi wa Somalia, na mkuu wa kikosi cha polisi cha Somalia, Sharif Sheikhuna Maye, kama sehemu ya juhudi za vikosi vya washirika za kuufanya mji uwe na salama, maafisa walikiambia kituo cha redio.

Maye aliwataka wakazi wa Afgoye kufanyakazi pamoja na vikosi vya usalama kufuata sharia na kanuni. Alisema polisi wa Somalia wanaelewa kuwa washirika wa al-Shabaab wapo katika ushoroba wa Afgoye na kuwataka watu kuwaarifu viongozi kwa tukio lolote linalotia shaka.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 3)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo