Red_arrow

Ungependa kuifanya Kiswahili kuwa lugha ya chaguo lako, katika tovuti hii? |

Kenya kufunga kamera zilizounganishwa na televisheni

Mei 24, 2012

  • 1 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Karibuni Kenya itaanza kufunga kamera zilizounganishwa na televisheni (CCTV) mjini Nairobi ili kuwasaidia polisi na kuimarisha usalama, Waziri Mkuu Raila Odinga aliliambia bunge hapo Jumatano (tarehe 23 Mei).

“Kufungwa kwa CCTV kutasaidia polisi katika kazi yao ya ulinzi kwa sababu wataweza kuwabaini wahalifu wakati wakitembea kujaribu kufanya uhalifu au baada ya kwisha kuufanya wanaweza kukamatwa haraka,” Odinga alisema, kwa mujibu wa Redio Capital FM News ya Kenya.

Mpango wa CCTV baadaye utapanuliwa na kupelekwa kwanza Mombasa, Kisumu, Eldoret, Nakuru na Meru, alisema. Serikali ya China imetoa shilingi bilioni 8.5 (dola milioni 100) ili kugharamia mradi huo, na Kenya imetenga shilingi bilioni 1.7 za ziada (dola milioni 20) za mchango.

Msaidizi Waziri wa Tawala za Mikoa na Usalama wa Ndani, Joshua Orwa Ojode mapema mwezi huu aliliambia bunge kuwa serikali itawekeza katika kamera zilizounganishwa na televisheni ili kuimarisha usalama wa nchi kufuatia mashambulizi mawili ya karibuni ambapo watu wawili waliuawa na saba kujeruhiwa.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 5)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • Kate
    November 29, 2012 @ 05:51:15AM

    Msaidizi Waziri wa Tawala za Mikoa na Usalama wa Ndani si Josua Orwa Ojode

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo