Mei 24, 2012
Vikosi vya majeshi ya Somalia na wale wa Umoja wa Afrika (AMISOM) wanakaribia kwenye mji wa Afgoye unaodhibitiwa na wapiganaji wa al-Shabaab, alisema msemaji wa AMISOM hapo Jumatano (tarehe 23 Mei).
“Vikosi vinaaendelea vizuri na opresheni inakwenda kama ilivyopangwa,” alisema msemaji Luteni Kanali Paddy Ankunda aliiambia Mtandao wa habari wa Shabelle, akiongeza kusema kwamba hivi karibuni watachukua uongozi wa wilaya hiyo. Amesema vikosi visaidizi viko umbali wa kilometa 30 kaskazini magharibi mwa Mogadishu. Amewataka wakaazi wa eneo hilo kubakia majumbani mwao.
Vikosi vya washirika vimepiga "hatua nzuri", kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na vikosi hivyo siku ya Jumatano.
Lengo la “Operesheni huru ya Shabelle” ni kuwapa ulinzi watu 400,000 wa eneo la Afgoye”, makaazi ya kundi kubwa la watu hao waliotawanyika kwa kiasi kikubwa duniani, ilisema taarifa hiyo.
Kamanda mwandamizi wa al-Shabaab na kikosi chake cha ulinzi waliuawa wakati wa mapigano ya siku ya Jumanne, ilisema taarifa hiyo.
"Operesheni hiyo imeendelea kufanya vizuri. Magaidi wa al-Shabaab wanakimbia,” alisema Luteni Jenerali Andrew Gutti. “Wanajua kuwa wanapoteza mwelekeo, na pia wanapoteza marafiki katika maeneo mbalimbali ya Somalia. Tunatoa wito kwa watu wa mji wa Afgoye kutoa sehemu za kigeni zinazobaki maeneo mwao.”
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
Mahakama moja ya Bosaso iliwatia hatiani na kuwapiga faini Wairani 78 siku ya Jumapili (tarehe 19...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata watuhumiwa 15 kuhusiana na kulichoma Kanisa la Bethania kweny...
Mkuu wa Polisi wa Kenya, David Kimaiyo, ameondoa nafasi za afisa polisi wa jimbo, afisa wa upelel...
Watu wenye silaha waliwaua watu wawili na kuwajeruhi wengine wanne katika mashambulizi tofauti kw...
Mkutano wa kuzungumzia uwezekano wa uchimbaji mafuta na gesi, uwekezaji, usalama na miundombinu n...
Wizara ya Masuala ya Wanawake na Familia ya Puntland ilianza mafunzo ya siku nane hapo Juampili (...
Zaidi ya Wasomali milioni 1 hawatakuwa na "usalama wa chakula" hadi mwezi wa Septemba, Mtandao wa...
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji