Wapiganaji wa al-Shabaab 40 waasi, wajisalimisha kwa serikali ya Somalia

Mei 22, 2012

  • 1 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Zaidi ya wapiganaji 40 wa al-Shabaab huko Somalia ya Kati waliasi na kujisalimisha kwa vikosi vya serikali na Ahlu Sunna wal Jamaa, Shirika la Habari la Taifa la Somalia liliripoti Jumanne (tarehe 22 Mei).

Wengi wa wapiganaji hao wanatokea Galgadud, ambapo vikosi vya Serikali ya Mpito ya Shirikisho vipo katikati ya kampeni ya kuwaondoa al-Shabaab.

“Wapiganaji hawa walituita mwanzoni mwa mwezi Aprili na kutuomba msaada. Tuliwaahidi kuwasaidia kutoka katika kundi la al-Shabaab na tulifikia mwisho wa makubaliano yetu,” Kiongozi wa operesheni za jeshi la Ahlu Sunna wal Jamaa katika wilaya ya El Bur Abdi Hassan Mohamed aliliambia shirika rasmi la habari. “Tunawakaribisha, kwa kuwa ni watoto wetu ambao walioshauriwa vibaya.”

Wapiganaji hao walikataa ukatili na al-Shabaab dhidi ya raia wa Somalia.

Katika tukio tofauti, wapiganaji 10 wa al-Shabaab waliripotiwa kulihama kundi hilo na kujisalimisha kwa vikosi vya usalama katika mkoa wa Hiraan.

Waziri wa Ulinzi wa Somalia Hussein Arab Isse alisema kuwa mpiganaji yeyote wa al-Shabaab ambaye ataasi na kujiunga na serikali atapewa uangalizi kamili wa maisha.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 18)

Dislike_icon(7)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • nok
    June 14, 2012 @ 06:26:01AM

    Ni vyema kuwa wanamgambo wa al-Shabaab sasa wanatambua makosa yao baada ya nguvu kutumika. Hii inathibitisha imani yangu kuwa "ikiwa demokrasia imeshindwa, huna njia nyingine isipokuwa kutumia nguvu."

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo