Mei 18, 2012
Polisi wa Kenya walisema Ijumaa (tarehe 18 Mei) kuwa wanamtafuta mwanaume wa Kijerumani wakitaka kumhoji kuhusu ushirikiano wa al-Shabaab wa Somalia waliowashirika na al-Qaeda.
Polisi wa Kenya mwishoni mwa wiki iliyopita walianza kumsaka Ahmed Khaled Mueller, aliyezaliwa Bonn, wakisema anaweza kuwa na taarifa kuhusu shughuli zilizopangwa na al-Shabaab.
Mnamo Jumatano, polisi walisema wamemkamata mwanaume ambaye wanaamini kuwa ni mshukiwa wa Kijerumani, lakini hawakuwa wamemtambua rasmi. Mwanaume huyo aligundulika kuwa raia wa Ujerumani lakini sio yule wanayemtafuta, alikamatwa kwa mashtaka ya dawa za kulevya, kwa mujibu wa AFP. Maofisa wa Polisi wa Kenya walisema msako wa Mueller unaendelea.
Kenya imekuwa ikikumbwa na mashambulio kadhaa toka ilipotuma vikosi kwenda Somalia ya kusini Oktoba 2011 kupambana na al-Shabaab.
Huko Mombasa, mlinzi wa usalama aliuawa na watu watano kujeruhiwa wakati mtu mwenye silaha alipofyatua risasi kwenye mgahawa wa Belle Vista Jumanne.
Polisi wa Kenya walitoa tahadhari kuwa Mueller anaweza kuwa na silaha na inaaminika pia anatumia majina ya Andreas Martin Muller na Abu Nusaibah.
Polisi waliwakamata mamia ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa al-Shabaab katika wilaya za Hod...
Kongamano la siku tatu juu ya elimu lilifunguliwa mjini Mogadishu siku ya Jumanne (tarehe 18 Juni...
Wanajeshi wa serikali ya Somalia wakisaidiwa na wanajeshi wa Misheni wa Umoja wa Mataifa (AMISOM)...
Waziri wa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa, Joseph Ole Lenku, siku ya Jumatatu (t...
Moto kwenye soko kubwa la Garissa uliharibu zaidi ya maduka 100 usiku wa Jumatatu (tarehe 17 Juni...
Waziri wa Umoja wa Kitaifa wa Djibouti Zahra Youssouf Kayad alisaini mikataba ya miradi miwili ye...
Kamati ya bajeti ya Bunge ya Kenya imekataa pendekezo la kununua ofisi mpya kwa aliyekuwa Rais Mw...
Moto ulifanya uharibifu mkubwa katika mji wa Balbala huko Djibouti siku ya Jumapili (tarehe 16 Ju...
Picha ambazo al-Shabaab ilizituma siku za Jumapili (tarehe 16 Juni) kwenye mtandao wa Twitter za ...
Polisi nchini Kenya walimuua mtuhumiwa wa ugaidi, Kassim Omolo Otemo, mjini Mombasa wakati uvamiz...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji