Vikosi vya Somalia vyakaribia Hudur, washukiwa wa al-Shabaab wakamatwa

Mei 17, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Vikosi vya usalama vya Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia vinakaribia ngome ya al-Shabaab katika wilaya ya Hudur ya kusini mwa Somalia, mbunge wa Somalia Ahmed Sheikh Mohammed aliuambia mtandao wa Shabelle Media Network siku ya Alhamisi (tarehe 17 Mei).

Kama Mungu akipenda, tutachukua sehemu iliyobakia inayomilikiwa na waasi karibu na Hudur hivi punde kutoka kwa wapiganaji wa al-Shabaab,” Mohammed alisema. “Tuko umbali wa kadri ya kilometa 10 tu.”

Katika habari zinazohusiana na hizo, vikosi vya usalama vya Somalia huko Dhobley mnamo Jumatano vilimkamata mwanamke na wanaume wawili wanaotuhumiwa kufanya mipango ya kushambulia eneo hilo na jirani Kenya, Redio Bar-Kulan inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa iliripoti.

Washukiwa hao ilisemekana wako katika hatua za mwisho za kupanga mfululizo wa mashambulio, kwa mujibu wa ofisa wa serikali ya Dhobley, Hanad Farah. Farah alisema serikali hiyo itaendelea kuchukua hatua kali za kinidhamu dhidi ya wapiganaji wa al-Shabaab wanaoshukiwa na wafuasi wao.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 2)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo