Mpango wa Chakula Duniani watoa mbadala wa vyakula vibichi kwa Somaliland

Mei 16, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wameanza mradi mpya nchini Somaliland kuwapa maelfu ya watu vocha za kununua nyama mbichi na vyakula kutoka kwa wauzaji wa ndani, Umoja wa Mataifa ulitangaza siku ya Jumanne (tarehe 15 Mei).

"Kutumia vocha kunawapa watu uchaguzi wa chakula gani cha kukiwa na kutoa nyenzo mpya yenye nguvu kwa WFP kwa ajili ya kutoa msaada wa chakula kwa wale waliopo katika mazingira magumu zaidi," alisema Mkurugenzi wa WFP nchini Somalia Stefano Porretti. "Wakati huohuo, vocha zinasaidia uchumi wa nchi kwa kuwasaidia wazalishaji wadogo na wa kiwango cha kati na wachuuzi wa nchini."

Wasomali 15,000 waliosajiliwa katika programu hiyo watapokea Dola za Marekani 80 kwa vocha kila mwezi, ambazo wanaweza kutumia katika ununuzi wa mchele, mafuta ya kula na nyama. WFP ina mpango wa kupanua programu ambayo inasemekana kuwa imefanikiwa kuwa mbadala wa uwiano wa chakula.

WFP inashirikiana na Baraza la Wakimbizi la Denmaki kusambaza vocha hizo, kwa kushirikiana na Medair, asasi isiyo ya serikali ambayo inasimamia programu ya lishe huko Burao, ambako awamu ya kwanza ya programu ya vocha imeanza.

WFP imepanga kutumia programu ya vocha katika nchi nzima, ambako hali ya soko inaruhusu.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo