Mei 16, 2012
Polisi wa Kenya walimkamata mwanaume anayeshukiwa kuwa amehusika katika shambulio la bomu katika mgahawa huko Mombasa ambalo lilimuua mwanamke mmoja na kujeruhi watu watatu, Mkuu wa Polisi Mathew Iteere aliwambia waandishi wa habari Jumatano (tarehe 16 Mei).
Katika shambulio hilo la Jumanne jioni, mwanaume mwenye silaha alipiga risasi mgahawa wa Vista Belle, wakati walinzi wa usalama walipomzuia na washiriki wake wawili kutoingia katika mgahawa huo. Washiriki hao wawili katika jinai hiyo walirusha mabomu kwenye mgahawa huo na kukimbia.
Moja ya bomu lililipuka karibu na mlango wa kuingia kwenye mgahawa na lingine karibu na sehemu ya maegesho ya magari nje.
Tumempoteza mmoja wa waathirika, msichana ambaye alikuwa mlinzi wa klabu hii, alifia hospitalini,” mkuu wa polisi wa kanda Aggrey Adoli aliiambia AFP.
Majeruhi watatu wamebakia hospitali, mmoja ana hali mbaya. “Mshukiwa huyo ni mmoja wa wale waliojeruhiwa,” Iteere alisema. “Kwa sasa yuko chini ya ulinzi wa polisi."
Mshukiwa alikuwa amekata tiketi ya basi kuondoka Mombasa mara tu baada ya shambulio, Iteere alisema.
“Tumeipata tiketi ya basi na wakati maofisa wetu walipokwenda kituo cha basi, waliikuta mizigo yake, ambayo ilikuwa na bunduki iliyokuwa imejazwa mizunguko minane ya risasi," alisema. "Pia tulipata kompyuta ya mkononi kutoka kwake ambayo sasa tunaichunguza.”
Iteere alisema polisi wamekuwa wakimtafuta mshukiwa “kuhusiana na mashambulio mengine kadhaa”.
Hakuna kundi lililodai kuhusika, ingawaje Kituo cha Vijana wa Kiislamu cha Kenya, kundi linalohusishwa na al-Shabaab, wanaelekea kufanya shambulio hilo.
"Asubuhi hii, nani wanafurahi na nani wanaoomboleza? Fikiria kuhusu jambo hili. Tokeni Somalia!” ujumbe mmoja katika mtandao wa Twitter ulisomeka hivyo. Bomu moja au mawili katika eneo sahihi na sauti yake husikika kwenye uchumi wa Kenya.”
Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, alisema kazi za Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alipokea vyeti vya utambul...
Kwa uchache watu wanne waliuawa na watatu kujeruhiwa siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) baada ya wa...
Kenya na Tanzania zilifanya operesheni ya pamoja ya ulinzi wa mpaka siku ya Alhamisi (tarehe 16 M...
Mwanachama wa kundi la wanamgambo wanaoiunga mkono serikali ya Somalia la Ahlu Sunna wal Jamaa, A...
Wanawake watatu waliuawa usiku wa Alhamisi (tarehe 16 Mei) katika eneo la Malkamau kwenye Kaunti ...
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon. siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alimteua waziri wa...
Tanzania na Canada zimesaini mkataba wa ushirikiano yanayokusudiwa kuimarisha na kuunda mazingira...
Jeshi la Taifa la Somalia liliwauwa wanamgambo 13 wa al-Shabaab siku ya Jumanne (tarehe 14 Mei), ...
Muda wa mwisho kwa wakaazi wa Mandera kusalimisha silaha zao haramu umeongezwa hadi Ijumaa (tareh...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Haya ni matendo ya uoga na matendo kama haya msiyavumilie.