Umoja wa Mataifa: Somalia inakabiliwa na ‘fursa kubwa’ ya kuhitimisha kipindi cha mpito

Mei 16, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia ametoa wito kwa jumuiya za kimataifa Jumanne (tarehe 15 Mei) kuongeza jitihada zake katika kusaidia Somalia kuhitimisha kipindi cha mpito.

“Kwa kuwa Somalia inakabiliwa na fursa kubwa ya kuhitimisha mpito, baada ya uwekezaji mkubwa wa Jumuiya za kimataifa na wanaoitakia heri Wasomali, ni lazima tukamilishe kazi hii tuliyo nayo mkononi,” Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu kwa Somalia Augustine P. Mahiga aliiambia Baraza la Usalama huko New York. “Lazima tutoe mpangilio wa ugavi na usafirishaji wa watu na vitu kwa wakati na msaada wa fedha kutuwezesha kukamilisha utekelezaji wa Mpango kabla ya Agosti mwaka huu, pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na uratibu.”

“Ukosefu wa fedha kwa Mpango huu katika miezi mitatu iliyobakia ni kero muhimu kwa sisi sote, ikijumuisha Serikali ya Mpito ya Shirikisho,” alisema. “Bunge la Katiba linakaribia kusaga meno kwa kukosa fedha.”

Mjumbe huyo alirudia kusema kuwa waharibifu wanaweza kuharibu mambo yaliyokwishafanywa kuelekea kwenye ujenzi wa amani nchini Somalia. “Lazima tushughulikie vipengele hivi kabla hawajafanikiwa kurudisha nyuma mchakato wa amani,” Mahiga alisema.

Somalia inakumbana na tarehe ya mwisho ya utekelezaji wa Mpango Mkuu tarehe 20 Agosti.

Baraza la Usalama lilisema kuwa muda unakwisha, mchakato wa siasa kwa sasa uko katika "awamu ngumu”. Wajumbe wa Baraza walisifu maendeleo yaliyokwishafanywa hadi sasa, lakini “wakielezea wasiwasi kuwa baadhi ya tarehe za mwisho za ukamilishaji wa kazi tayari zimeshapita.”

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa wa Ufaransa Gerard Araud vilevile alielezea wasiwasi kuwa kila tarehe za mwisho za siasa zimebakiwa na wiki kadhaa.

“Kuchelewa kokote au upotoshaji katika utekelezaji wa mpito hautakubalika kabisa,” Balozi wa Marekani Susan Rice aliliambia Baraza hilo. “Somalia na kanda hiyo kubwa haitaweza kukubali kurejea katika hali ya kwanza ya vurugu na mateso ambayo yalikera nchi hii na kuwa tishio kwa kanda hii kwa miongo.”

Naye naibu Balozi wa Umoja wa Mataifa wa Uingereza Philip Parham alisema jumuiya za kimataifa ni lazima zisaidie jitihada ambazo zinatoa motisha katika maendeleo” na ambazo zimeandaliwa kuchukua hatua dhidi ya yeyote anayetafuta kuzuia au kufifisha mchakato huo”.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 1)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo