Askari 603 wa Somalia wamaliza mafunzo nchini Uganda

Mei 15, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Zaidi ya askari 600 wa Somalia walimaliza mafunzo ya kijeshi ya miezi sita nchini Uganda hapo tarehe 10 Mei na wanarejea nyumbani ili kukuza vikosi vya usalama vinavyopambana na al-Shabaab.

Kanali Winston Byaruhanga, mkuu wa shule ya mafunzo ya kijeshi ya Bihanga katika wilaya ya Ibanda, aliiambia idara ya habari ya IRIN kuwa mpaka mwisho wa mwaka, kiasi cha askari 3,000 na maafisa watapatiwa mafunzo ya kijeshi. Alisema kuwa askari 603 wa Somalia waliopatiwa mafunzo na askari 248 wa Uganda watasaidia kuleta amani na utulivu nchini Somalia.

“Askari hawa wanaunda sehemu muhimu ya jeshi la Somalia. Waambie al-Shabaab wako wapi, nao wako tayari kwa kazi,” alisema Luteni Jenerali Edward Katumba Wamala, kamanda wa Vikosi vya Miguu vya Uganda. “Askari hawa wataleta amani nchini Somalia. Sisi tuna msimamo hasi kuwa amani itapatikana Somalia karibuni.”

Mafunzo hayo ni pamoja na mazoezi ya vita vya mjini, kufahamu mabomu ya kuzikwa, afya, elimu ya siasa na silaha.

“Tumedhamiria kurejea nyumbani na kulinda amani nchini kwetu kutoka kwa al-Shabaab,” alisema askari wa Somalia Mohammed Ali Hassan, aliyetambuliwa kama mwanafunzi bora wakati wa mafunzo. “Sasa tumeshajengwa na tuko tayari kwa vita.”

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 1)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo