Afisa wa Umoja wa Mataifa watoa wito wa kusaidia upatikanaji wa riziki kwa Somalia

Mei 13, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuendelea kuwasaidia watu wa Somalia kwa kujenga utoaji wenye ufanisi wa misaada ambao ulisaida sana katika njaa ya mwaka jana na kuelekeza katika kusaidia upatikanaji wa riziki.

“Hali ya njaa haiko tena Somalia, kwa kiwango kikubwa kutokana na utoaji misaada kwa ufanisi na mavuno mazuri katika mwanzo wa mwaka, lakini hali ya kibinadamu inaendelea kuwa ngumu,” Msaidi Katibu Mkuu kwa Masuala ya Ubinadamu Catherine Bragg alisema hapo Jumamosi (tarehe 12 Mei) baada ya ziara ya siku tano katika Somalia na Kenya.

Idadi ya watu wanaohitaji chakula imepungua kwa milioni 1.5, lakini bado watu milioni 2.5 wako “katika shida”, Bragg alisema.

Bragg, ambaye pia ni Makamo Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Misaada ya Dharura, alisema Umoja wa Mataifa ulikuwa unashirikiana na watendaji wengine muhimu, ikiwa ni pamoja na Uturuki na Mkutano wa Jumuiya ya Kiislamu, katika kutoa misaada nchini Somalia.

“Wafanyakazi wa misaada wenyeji na wa kimataifa wanaoshirikiana na Somalia wamethibitisha kuwa wanaweza kufanya mambo kuwa tofauti,” alisema.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo