Mei 13, 2012
Mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa yamesaini taarifa ya makubaliano na serikali ya Somalia siku ya Ijumaa (tarehe 11 Mei) kuomba uimarishaji wa haki za binadamu nchini, Redio Bar-Kulan inayodhibitiwa na Umoja wa Mataifa iliripoti.
Makubaliano hayo yalifikiwa kwa ombi la serikali ya Somalia, na yatarahisisha uimarishaji wa maeneo saba makuu, ikiwa ni pamoja na kuimarisha utawala wa sheria na usimamiaji wa haki, kuvilinda vikundi vinavyoweza kudhurika kirahisi – ikiwa ni pamoja na wanawake, watoto, watu wa ndani ya nchi waliokimbia makazi yao na waandishi wa habari – pamoja na utekelezaji wa mikataba ya kimataifa juu ya haki za binadamu.
“Msaada wa kiufundi utatolewa katika njia ambayo itahakikisha umuliki wa kitaifa, ushiriki, uwazi na ujumuishaji wa wadau muhimu, hasa kuhusiana na vipaumbele vilivyokubaliwa katika kila eneo,” makubaliano hayo yanasomeka.
Makubaliano hayo yalitiwa saini huko Mogadishu na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Ofisi ya Kisiasa ya Umoja wa Matiafa Somalia na serikali ya Somalia.
Waziri Mkuu wa Somalia Abdiweli Mohamed Ali alielezea ahadi za serikali yake katika kuimarisha na kulinda haki za binadamu katika taarifa kwa waandishi wa habari baada ya kusaini makubaliano hayo.
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
Mahakama moja ya Bosaso iliwatia hatiani na kuwapiga faini Wairani 78 siku ya Jumapili (tarehe 19...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata watuhumiwa 15 kuhusiana na kulichoma Kanisa la Bethania kweny...
Mkuu wa Polisi wa Kenya, David Kimaiyo, ameondoa nafasi za afisa polisi wa jimbo, afisa wa upelel...
Watu wenye silaha waliwaua watu wawili na kuwajeruhi wengine wanne katika mashambulizi tofauti kw...
Mkutano wa kuzungumzia uwezekano wa uchimbaji mafuta na gesi, uwekezaji, usalama na miundombinu n...
Wizara ya Masuala ya Wanawake na Familia ya Puntland ilianza mafunzo ya siku nane hapo Juampili (...
Zaidi ya Wasomali milioni 1 hawatakuwa na "usalama wa chakula" hadi mwezi wa Septemba, Mtandao wa...
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji