Kukatika kwa usambazaji maji mjini Nairobi kuendelea

Mei 13, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Usambazi maji mjini Nairobi utaendelea kuathiriwa na kukatika katika kwa wiki mbili zijazo baada ya mafuriko kuharibu bomba kubwa kutoka bwawa la Sasumua kuelekea sehemu za kusini na magharibi ya jiji hapo Jumanne, Redio Capital News FM ya Kenya iliripoti hapo Jumamosi (tarehe 12 Mei).

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka Philip Gichuki aliwaambia waandishi wa habari kuwa maeneo yaliyoathiriwa yatapata maji kwa masaa 36 kila wiki. Alitoa tahadhari kwa wakazi wa mjini watumie maji kwa uangalifu, ingawa alihakikisha kuwa bei ya maji itabakia ile ile.

"Hili ni suala la dharura na tutabeba gharama ambazo zitatokea ingawaje hatuwezi kusema kwa sasa zitakuwa kiasi gani," alisema.

Maeneo yaliyoathiriwa ni pamoja na Karen, Westlands, Gigiri, Chuo Kikuu cha Nairobi, Lavington, Kawangware, Upperhill, Hospitali ya Taifa ya Kenyatta, Dagoretti Corner, Ngong Road Idara ya Ulinzi.

Bwawa la Sasumua ni la pili kwa ukubwa nchini, linalosukuma lita milioni 60 kwa siku na kutoa sehemu mbili kati ya tatu katika hifadhi ya maji ya Kabete kuelekea magharibi ya Nairobi.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo