Djibouti kufungua chuo kipya cha polisi

Mei 10, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Siku ya Jumanne (tarehe 8 Mei), baraza la mawaziri la Djibouti liliidhinisha mswaada wa sharia wa kuanzisha chuo cha polisi kitakachotoa mafunzo “katika kiwango cha juu”, liliripoti gazeti la nchi hiyo la La Nation hapo Jumatano.

Mswaada huo wa sharia uliwasilishwa kwenye mkutano wa baraza la mawaziri na waziri wa mambo ya ndani, Hassan Darar Houffaneh, na kukubaliwa moja kwa moja.

Chuo hicho kitatoa mafunzo kwa wanaume na wanawake kulitumikia taifa kwa kazi za upolisi na ulinzi, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu na kozi kwa wafanyakazi wengine wanaofanya kazi kwenye sekta ya usalama wa taifa.

Chuo pia kitafanya utafiti katika masuala ya usalama.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, serikali za majimbo ya shirikisho ziundwe vipi nchini Somalia kufuatia utata wa Jubbaland?

Angalia matokeo