Red_arrow

Ungependa kuifanya Kiswahili kuwa lugha ya chaguo lako, katika tovuti hii? |

Vikosi vya ushirika vya Somalia kupambana na al-Shabaab

Mei 10, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Kamati ya Usalama ya Pamoja ya Somalia Jumatano (tarehe 9 Mei) waliidhinisha pendekezo la kuunganisha vikosi shirika vya serikali kupambana na al-Shabaab na al-Qaeda, gazeti la Africa Review liliripoti.

Vikiosi hivi vitafanya kazi chini ya uongozi wa Wizara ya Ulinzi ya Somalia. Kamati hiyo ambayo hukutana kila baada ya miezi miwili, ina wawakilishi kutoka Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na Mamlaka kati ya nchi kwenye maendeleo miongoni mwao. Maofisa kutoka Puntland, Galmudug na Ahlu Sunna wal Jamaa walihudhuria pia.

Waziri Mkuu Abdiwel Mohamed Ali ambaye alikuwa mwenyekiti wa mkutano huu aliupitia mpango huo akisema amri kutoka makao makuu ya jeshi itaweza kuongoza vikosi hivyo.

Waziri wa Ulinzi wa Somalia Hussein Arab Issa aliwaambia waandishi wa habari baada ya kikao hicho kuwa washiriki wametoa wito kwa ajili ya kuunda makambi ya jeshi kuwa wenyeji wa vikosi vipya vya pamoja.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 2)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, serikali za majimbo ya shirikisho ziundwe vipi nchini Somalia kufuatia utata wa Jubbaland?

Angalia matokeo