UK yapunguza jitihada dhidi ya uharamia

Mei 09, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Uingereza imerudisha nyuma jitihada zake dhidi ya uharamia na haitaendelea kupeleka manowari ndogo ya doria mwaka mzima kupambana na kuwaondoa maharamia pwani ya Somalia, gazeti la The Guardian la Uingereza liliripoti Jumanne (tarehe 8 Mei).

Licha ya kukatisha, kupambana na uharamia pwani ya Somalia kutabaki kuwa kipaumbele kwa serikali ya UK. “Serikali itabakia kuwajibika kikamilifu kusaidia kurejesha utulivu nchini Somalia, na shughuli za Jeshi la Majini la Kifalme kuzuia na kuharibu utaratibu wa maharamia ni sehemu tu ya mtazamo kamili wa Uingereza,” Waziri wa Ulinzi wa Uingereza alisema.

Mkakati wa Ulinzi na Uhakiki wa Usalama wa mwaka 2010 unaondoa safari za manowari nne kutoka Jeshi la Majini la Kifalme ikaacha mbili kwa ajili ya operesheni za dharura mashariki ya Mfereji wa Suez. Huko nyuma Uingereza ilikuwa ikituma manowari nne pwani ya Somalia, zilizowekwa tayari kwa vita kwa mwaka mzima.

Mataifa kadhaa ya EU ikiwemo Ufaransa, IItalia na Denmaki zilijitolea kupeleka meli kupambana na uharamia pwani ya Somalia. Mwaka uliopita, mashambulio ya uharamia yaliyofanikiwa yalipunguzwa katika bahari ya Hindi kwa mujibu wa Kikosi Maji cha Umoja wa Ulaya nchini Somalia.

Ofisi wa Mambo ya Nje wa Uingereza ililiambia gazeti hili kuwa inafanya kazi ya “kuweka mtandao wa vituo vya kikanda huko Kenya, Morisi, Ushelisheli na Tanzania kuendesha mashtaka ya maharamia wa Somalia wanaoshukiwa ambao iwapo watapatikana na hatia watarudishwa Somalia kutumikia vifungo vyao katika magereza salama na inayojali ubinadamu.

Mwezi uliopita serikali ya Ushelisheli iliwahamisha maharamia 17 kwenda kutumikia vifungo vyao huko Somaliland, wakikidhi makubaliano ya pande mbili yaliyofikiwa Februari.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo