Mei 09, 2012
Waziri wa Ulinzi wa Somalia Hussein Arab Isse alisema Jumanne (tarehe 8 Mei) kuwa Serikali ya Mpito ya Shirikisho (TFG) hivi karibuni watawaondoa kabisa al-Shabaab katika nchi hiyo.
Isse alisema malengo ya TFG yalikuwa kurejesha amani katika kanda na kuwaondoa al-Shabaab Somalia ya kati na Kusini ikiwa ni hatua moja muhimu katika kuelekea kwenye kufikia lengo hilo.
“Ingawaje wameondoka Mogadishu, haimanishi kwamba tuanze kusinzia,” alisema, kwa mujibu wa Mtandao wa Habari wa Shabelle Media Network ya Somalia. “Vikosi vyetu vitaendelea kupambana na al-Shabaab."
Isse alisema mbinu za al-Shabaab zimebadilika kuwa za kulenga raia kutoka TFG walipochukua udhibiti wa Mogadishu mwaka uliopita, na kutoa wito kwa Wasomali kushirikiana na vikosi vya TFG kuepusha mashambulio zaidi.
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
Watu watano waliuawa na wanne kujeruhiwa katika mashambulizi mawili kwenye eneo la kaskazini mash...
Sababu kuu ya vurugu ambazo ziliua zaidi ya watu 150 katika Delta ya Mto Tana mwaka jana ilitokan...
Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza mlipuko wa polio katika Pembe ya Afrika siku ya Jumatan...
Majeshi ya serikali ya Somalia yamezifungia kampuni za mawasiliano ya simu na biashara nyingine h...
Serikali ya Somalia itaanza kuunda tawala za kikanda katika maeneo yaliyokombolewa kutoka kwa al-...
Waziri wa Nishati wa Djibouti Ali Yacoub Mohamoud na Balozi wa Japani nchini Djibouti Atsushi Nis...
Ufunguzi wa Mkutano wa Wasambazaji wa mafuta na gesi Tanzania utafanyika huko Dar es Salaam tareh...
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Hongereni wananchi wa somalia kwa kukubali amani itawale,hongereni pia serikali ya mpito ya somalia umefanya kazi kubwa sana,nipende pia kuwapongeza umoja wa Afrika kwa kutuma wanajeshi ili kurudisha amani,Mungu atawalipa kwa kujitolea maisha yenu ili ndugu zetu wa somalia waonje uzuri wa amani kama yalivyo mataifa mengine.Mungu ibariki somalia Mungu ibariki Afrika
Tunamshukuru Waziri wa Ulinzi Isse kwa msimamo wake wa kuwang’oa al-Shabaab kutoka Somalia na mbinu zao chafu za kuwalenga wananchi na kuwasababishia hali ngumu wale wasiohusika na vikundi vya kisiasa nchini Somalia. Asante waziri, tunatumai hatimaye utamshinda adui yako na nchi yote itawakamata pamoja na eneo lote kwa jumla.
Al-Shabaab ni kikundi cha kihuni kinachofanya shughuli zake ndani ya Somalia na tangu kilipoanza kimeacha alama ya vifo na uharibifu kila kinapokwenda. Vitendo vyao vinakosolewa na ulimwengu mzima na watu wengi wanaamini kuwa lazima wasitishwe kwa gharama yoyote ile. Wanakwenda kinyume na haki za binadamu kwa kuteka nyara watoto wenye umri chini ya miaka 18 na kuwapa mafunzo ya uaskari ili wapigane kwa sababu ambayo hata hawaijui. Wanaua wananchi wasio na hatia Somalia na nchi jirani. Pia wanashambulia misafara ya kibinadamu na kuwazuia wasifike sehemu zilizokumbwa na njaa na magonjwa. Kutokana na vitendo vyao, Wasomali zaidi na zaidi wataendelea kufa kila siku ikiwa hawatasitishwa. Kikundi hiki cha kigaidi kinasababisha mwenendo wa ukuaji wa uchumi nchini kudorora kwa sababu watu wanahofia maisha yao kutokana na mashambulizi mfululizo hakuna kitakachoendelea.