Serikali ya Kenya yasambaza misaada ya miradi ya dijitali

Mei 08, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Serikali ya Kenya imegawa shilingi milioni 106 (Dola za Marekani million 1.3) kwa kampuni za teknolojia nchi nzima ili kuhimiza maendeleo ya maudhui ya dijitali, gazeti la Daily Nation la Kenya liliripoti Jumatatu (tarehe 7 Mei).

Zaidi ya mashirika 30 yaliteuliwa kutoka katika maombi 790 ya fedha. Mashirika yatafanya kazi ya kubadilisha mihutasari ya shule kuwa katika mfumo wa dijitali na kuanzisha michezo ya video na programu za sekta ya afya.

"Sasa tumeacha kujadili miundombinu hadi kwenye maendeleo ya maudhui, sera nzuri na kujenga uwezo wa tasnia," alisema Katibu Mkuu wa Habari na Mawasiliano Bitange Ndemo.

Mradi wa kugharamia maudhui ya dijitali ni sehemu ya msaada wa shilingi milioni 250 (Dola za Marekani milioni 3) kutoka Benki ya Dunia, ambao unakusudia kuhamasisha ugunduzi wa kiteknolojia wa wenyeji.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo