Mei 08, 2012
Taarifa ya utafiti uliotolewa na Chama cha Walipakodi cha Taifa Kenya siku ya Jumatatu (tarehe 7 Mei) uligundua kwamba kuimarishwa kwa uchunguzi wa umma na mashtaka ya watuhumiwa wa ubadhilifu wa mali ya umma umepunguza matumizi mabaya ya fedha.
Hata hivyo, taarifa hiyo ilionyesha kwamba shilingi milioni 363 (Dola za marekani milioni 4.3) zilitumika vibaya katika mwaka wa fedha wa 2009-2010, gazeti la Business Daily Africa liliripoti.
Chama hicho kilifanya utafiti wa majimbo 38 na kiligundua kwamba jimbo la uchaguzi la Gatanga lilikuwa la kwanza kwa matumizi mazuri ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo (CDF) na Mfuko wa Kuhamisha Mamlaka ya Ndani, bila kuwa na tukio la matumizi mabaya ya fedha.
Wundanyi, lilikuwa ni jimbo la pili ambalo mbunge wake alipongezwa kwa kuruhusu wapiga kura kuchagua wajumbe wa kamati ya CDF. "Kila kundi limewakilishwa, ndiyo maana tuna utendaji mzuri," mbunge wa Wundanyi Thomas Mwadeghu alinukuliwa akilieleza gazeti la Daily Nation la Kenya.
Marakwet Mashariki lilikuwa ni jimbo lililofanya vibaya kuliko yote kwa takriban asilimia 50 ya fedha za CDF hazikutumika vizuri.
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
Mahakama moja ya Bosaso iliwatia hatiani na kuwapiga faini Wairani 78 siku ya Jumapili (tarehe 19...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata watuhumiwa 15 kuhusiana na kulichoma Kanisa la Bethania kweny...
Mkuu wa Polisi wa Kenya, David Kimaiyo, ameondoa nafasi za afisa polisi wa jimbo, afisa wa upelel...
Watu wenye silaha waliwaua watu wawili na kuwajeruhi wengine wanne katika mashambulizi tofauti kw...
Mkutano wa kuzungumzia uwezekano wa uchimbaji mafuta na gesi, uwekezaji, usalama na miundombinu n...
Wizara ya Masuala ya Wanawake na Familia ya Puntland ilianza mafunzo ya siku nane hapo Juampili (...
Zaidi ya Wasomali milioni 1 hawatakuwa na "usalama wa chakula" hadi mwezi wa Septemba, Mtandao wa...
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji