Mei 07, 2012
Mwanariadha wa Kenya, Dennis Kimetto, ameweka rikodi mpya ya dunia hapo Jumapili (tarehe 6 Mei) kwa mbio za kilomita 25 kwenye Uwanja wa Olimpiki wa Berlin, Ujerumani, akitumia saa 1, dakika 11 na sekunde 18.
Kimetto, mwenye umri wa miaka 28 aliivunja rikodi iliyowekwa na Mkenya mwenzake Sammy Kosgei miaka miwili iliyopita huko Berlin kwa kukimbia kwa saa 1, dakika 11 na sekunde 50.
Kimetto alikimbia sambamba na Wakenya wengine wawili, Wilfred Kigen na Jacob Kendagor, ambao walipata nafasi za pili na tatu. Kigen pia alivunja rikodi ya hapo kabla kwa kukimbia kwa saa 1 dakika 11 na sekunde 29.
“Ilikuwa lengo letu kuvunja rikodi,” alisema Kimetto, kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Riadha. “Tulijua ndani ya mashindano yote kuwa tutaweza kufanya hivyo.”
Mkenya Caroline Chepkwony, mwenye umri wa miaka 27, alichukuwa nafasi ya kwanza katika mbio za wanawake akitumia saa 1, dakika 22 na sekunde 56.
“Hili ni jambo kubwa na lilikuwa la kasi sana. Nilikimbia kwa dakika moja mbele zaidi kuliko nilivyopanga,” alisema Chepkwony.
Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, alisema kazi za Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia ...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alipokea vyeti vya utambul...
Kwa uchache watu wanne waliuawa na watatu kujeruhiwa siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) baada ya wa...
Kenya na Tanzania zilifanya operesheni ya pamoja ya ulinzi wa mpaka siku ya Alhamisi (tarehe 16 M...
Mwanachama wa kundi la wanamgambo wanaoiunga mkono serikali ya Somalia la Ahlu Sunna wal Jamaa, A...
Wanawake watatu waliuawa usiku wa Alhamisi (tarehe 16 Mei) katika eneo la Malkamau kwenye Kaunti ...
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon. siku ya Alhamisi (tarehe 16 Mei) alimteua waziri wa...
Tanzania na Canada zimesaini mkataba wa ushirikiano yanayokusudiwa kuimarisha na kuunda mazingira...
Jeshi la Taifa la Somalia liliwauwa wanamgambo 13 wa al-Shabaab siku ya Jumanne (tarehe 14 Mei), ...
Muda wa mwisho kwa wakaazi wa Mandera kusalimisha silaha zao haramu umeongezwa hadi Ijumaa (tareh...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji