Waziri wa mipango wa Somalia amepokea ujumbe wa Shrika la Chakula Duniani

Mei 07, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Waziri wa Mipango na Ushirikiano wa Kimataifa wa Somalia, Abdullahi Godah Barre, alimpokea mjumbe wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Stefano Porretti, hapo Jumapili (tarehe 6 Mei), liliripoti Shirika la Habari la Somalia.

Maafisa hao wawili walijadiliana mikakati ya kutoa misaada ya kibinaadamu katika msimu wa mvua unaokuja, hasa katika njia bora kabisa za kupunguza athari mbaya za mvua hizo kwa watu wanaoishi kwenye makambi wa wakimbizi, Barre aliwaambia waandishi wa habari baada ya mkutano.

Porretti aliishukuru serikali ya Somalia kwa ushirikiano wake na shirika la WFP wakati shirika hilo linapojitolea kuwasaidia watu walio kwenye mazingira magumu kupitia misaada ya chakula na misaada mengineyo. Alisema WFP iko tayari kuongeza juhudi zake kuwasaidia raia wa Somalia.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo