Yemen yatangaza kukamatwa kwa maharamia wa Kisomali 14

Mei 07, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Walinzi wa Mwambao wa Yemen waliwatia mbaroni washukiwa wa Kisomali 14 karibu na Kisiwa cha Socotra katika Ghuba ya Aden (tarehe 6 Mei), Wizara ya Ulinzi ya Yemen ilitangaza.

Wizara hiyo ilisema washukiwa wamepelekwa kwa mamlaka za usalama kwa uchunguzi.

Uharamia ni tatizo linaloendelea katika maji kati ya Somalia na Yemen, ikiwemo Ghuba ya Aden na katika bahari ya Uarabuni.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Yemen ilitangaza mwezi uliopita kuwa meli ya vita ya Hispania ilikuwa ikisaidia kuokoa wavuvu tisa wa Yemen kufuatia kutekwa na maharamia.

Mahakama ya kusikiliza makosa ya jinai ya Yemen ilitoa hukumu kwa maharamia wa Kisomali 10 kwenda jela miaka 10 mwezi Novemba mwaka uliopita baada ya kuwakuta na hatia ya uharamia katika maeneo ya bahari ndani ya mipaka ya nchi ya Yemen, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo